Jina la Tanzania linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika maandamano ya ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe kabambe za ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow, Scotland, uliobeba watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia live sherehe hizo kupitia katika TV zao. Takriban  mashabiki 100,000, na wanamichezo 4,000 kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana wapo hapo kwa michezo hiyo ambapo hii ni mara ya 20 kufanyika toka ianzishwe.
 Sehemu ya wanamichezo wa Tanzania kwenye sherehe hizo za ufunguzi. Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada za Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand
 Tanzania Oyeeeee....!!!!
 Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Suleiman Mjaya Nyambui (T-shirt ya njano) akihamasisha vijana wake
Nahodha na bondia wa Tanzania Seleman Salum Kidunda akipeperusha juu bendera ya Taifa wakati akiongoza wenzake kwenye maandamano hayo ya ufunguzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2014

    Kushiriki sio kumeremeta.Kushinda ndiko kunakohitajika na ndipo pale uwanja utameremeta ukisikika kwa wimbo wa Taifa la Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2014

    Kila la kheri wabongo wenzetu peperusheni vema bendera yetu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2014

    Kila la kheri wabongo wenzetu peperusheni vema bendera yetu

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza kabisa, mimi naamini hata kushiriki tu peke yake, basi pia tuna haki ya kujisifia 'kumeremeta' na naamini kama tutajaaliwa kubahatika kupata huo ushindi uliouongelea, basi hapo itakuwa si kumeremeta tena, bali TUTANG'ARA kabisaaaaa!!!! Kwa nderemo, vifijo na sauti zikipaa kwa kuimba wimbo wa Taifa letu la Tanzania. Tujipe moyo naamini tutashinda. Mungu ibariki Tanzania ibariki na Team Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...