Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Habari zinasema kwamba hayo ni masalia ya viungo vya binadamu vilivyotupwa maeneo ya kutoka chuo kimoja cha udaktari (jina kapuni kwa sasa) baada ya wanafunzi kumaliza kutumia kwa mazoezi. Viungo hivi vilitupwa baada ya kukosa pesa za kuteketeza kwenye tanuri maalum. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anatarajiwa kuzungumza mchana huu juu ya sakata hilo.
Habari zinasema kwamba hayo ni masalia ya viungo vya binadamu vilivyotupwa maeneo ya kutoka chuo kimoja cha udaktari (jina kapuni kwa sasa) baada ya wanafunzi kumaliza kutumia kwa mazoezi. Viungo hivi vilitupwa baada ya kukosa pesa za kuteketeza kwenye tanuri maalum. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anatarajiwa kuzungumza mchana huu juu ya sakata hilo.
Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili
Jamani jamani jamani!!
ReplyDeleteDalili za kiyama hizo leo tumefika hapo tunaona kila jambo baya ktk macho yetu kila aina ya zambi kubwa kubwa zinafanywa bila kisisi kwa zambi ambazo tunazofanya naweza kusema hata kabla yetu hawakuwahi kufanya inasikitisha sana
ReplyDeleteKiukweli dunia imeisha ... Unyama umetawala yani dah!!
ReplyDeleteEeeeh Mungu ni wapi tuelekeako taifa hili!watu hawana hata chembe ya huruma!nahisi kulia na kuzzimia,Mungu tusaidie
ReplyDeleteKweli ukistaajabu ya Musa....
ReplyDeleteUuuwi maiti zote hizo zimetoka wapi? Naogopa mie
ReplyDeleteUuuuwiii
ReplyDeleteThe mdudu,ndugu zangu watanzania kwakweli nchi ilipofikia ni pabaya sn tena sn mauwaji kama haya enzi ya mwalimu nyerere utaanzia wapi? Yaani siku hizi mtu akipotea yaani kuanzia ndugu hadi mjumbe wa nyumba kumi hawajui? Hii ni hatari sn na ni janga la taifa,tukumbushane enzi za mwalimu kipindi kile mikusanyiko ya vijana kupiga domo la siasa ilikua marufuku na ilitusaidia sn kuondokana na jaziba za wanaadamu wasio na utu kwawezao lakini leo hii vijana wakiwa kwenye mikusanyiko baada ya pilika za mchana basi kinachofuata ni siasa kwenda mbele matokeo yake ndio haya tunayoyaona leo hii mtu anaongea siasa na jaziba juu mpaka povu linamtoka mdomoni akitoka hapo anaanza kumvizia mpinzani wake na kummaliza utasema yeye ndie aliemleta hapa duniani,,ndugu zanguni chonde chonde tubadilikeni tunalitia aibu taifa letu na chakushangaza watu haohao waliohusika wakitiwa mikononi mwa serikali kunatokea watu wanaojiita wanasheria nakuanza kuwatetea huu ni ujinga na upumbavu watu kama hao wakitiwa nguvuni ni kunyongwa au maisha jera,huku kuteteana kijingajinga ndio maana watu hawachoki au kuogopa kufanya kitu mbaya coz wanajiamini kuna watu watawatetea,,nimechefuka kweri moyoni kuona tunauwana kama wanyama
ReplyDeleteMmmh hadi tumbo linauma inatisha kwa kweli
ReplyDeletehii inaonyesha ni jinsi gani watu wanavyojali pesa kuliko utu na yote hii ni kwa sababu ya tofauti kubwa za kipato miongoni mwetu, kukamata na kuwaadabisha hawa ni njia moja wapo ya kudhibiti matukio kama haya lkn pia suluhu ya kudumu ni kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii tulionayo, ikiwemo pamoja na kugawanya rasilimali za taifa ktk uwiano unaolingana na kupambana na mmomonyoko wa maadili kwa kujenge tabia na utamaduni wa kujipatia kipato kwa njia halali na za haki,
ReplyDeletethis is too bad
Kwanini tanzania tusiwe na sheria kama china tunadumisha urafiki na china lakini hatufuati nyendo zao hao ni wakunyongwa tu na tena wakatwe katwe na wao ili iwe fundisho kwa wengine watakaofikria kufanya unyama kama huu aisee inaumaa sanaaa
ReplyDeleteWatanzania bwana....hivyo vimetumiwa na wanafunzi wanaosomea udaktari bila shaka..cjui kwann wamevetupa ovyo namna hiyo
ReplyDeleteMamboa kama haya yalikuwa na nguvu sana India na China na nchi nyingine za Asia mabako watu uvuna viungo kwa ajili ya kuuza (tansplant) kwa wagonjwa matajili: Mradi huu lazima kuna hospitali, madaktari na wenye ujuzi wa kuvuna viungo na kuvitunza vizuri, na pia kusafisha nje ya nchi: Fanya utafiti utaona kuwa ni mpango mzito "Mafia"
ReplyDeleteGari ni la nani?
ReplyDeleteNambari za usajili?
Dereva ni nani?
Yaani hakuna mtu aliyeweza kunusa hiyo harufu mbaya?
Vipande hivyo vilinyunyizwa dawa visioze au kutoa harufu mbaya?
Je, ni ushirikina?
Innallilahi waina ilahi rajiun! SubuhanaAllah wapi tunakoelekea wanaAdam hapo ndio Tunajiuliza security ya nchi ipo wapi? Kuanza uchunguzi mkubwa watu watangaze watu wao wanampotea DNA zifanye kazi hii Inatisha ndani ya nchi na Border kuwe na uchunguzi mkubwa na usalama wa Ulinzi. MZ
ReplyDeleteViungo vilikuwa vikitumiwa kama practical kwa wanafunzi wa udaktari.
ReplyDeleteAcheni kucheemka
Wahisi nani amechemka hapa?Hata kama miili hii ilitumika kama practical kwa wanafunzi maana ya utupwaji huo wa wazi kama mizoga ya Kunguru maana yake nini?Udhalilishaji wa binadamu haukubaliki kokote duniani labda Kichwani kwako tuu
DeleteMungu tusaidie.
ReplyDeleteIs this not medical waste?
ReplyDeleteUnaweza ukazimia kwakweli
ReplyDeleteKweli, mwacheni Mungu aitwe Mungu. Kweli ee kweli ee, Loo! nimegundua kwa nini watu wanakimbia Tanzania sasa kwa mtindo huu nyumbani hakufai loo! Ee Mola tuepushe
ReplyDeleteHaya sasa nyie mnaojiita ma doctor tupeni forensic mtuambie hao ni wa kina nanii? Au mtuambie bac wanawake ni wangapii na wanaume pia ndo tutajua kweliii bongo tuna ma doctor au wote mburulaz? Pia tunataka nyie viongoz wekeni tip line ili watu wajitokeze wawataje hao wahusika sio tuuu blah blah nyingiii zisizo na mafanikioo, fanyeni kazi mnaitia aibu nchi yetu Tanzania! !!!
ReplyDeleteHii yote inatokana na kutokuwa na viongoz waadilifuuu, n chi yetu haina viongoz shupavu swala kama hili wangechukua hatua za haraka kwa kaweka tip line kama Kuna mtu anajua mtu aliyefanya hivyo ajitokeze, ndo marekani huwa inafanya hivyo ili kupata muhusika kwa haraka, waweke dau la million 5 au 10 wa one kama hawato mpata muhusikaa, na sio blah blah nyingiii bila kutatua tatizo haisaidiiiii
ReplyDeleteNaona kuna na vifaa vingi vinavyotumika hospitalini (gloves) jambo linalonifanya niamini kuwa viungo hivyo vimetokea kataika moja ya hospitali kubwa hapa jijini. Huenda vinatokana na wagojwa kukatwa viungo hivyo kutokana na matatizo mbalimbali kama kusukari na mengineyo. Ila kwa nini wameamua kuvitupa kwa namna hiyo hilo ndio swala la kujiuliza.
ReplyDeleteMwenyezi mungu naomba utusaidie Tanzania.
ReplyDeleteKwanza kabisa, nimejiuiza sana, nahisi kuna mambo MATATU. 1). INAWEZEKANA HIVI VIUNGO VILIKUWA VINATUMIKA KATIKA MAZOEZI KWA VITENDO KWA MADAKTARI WETU, KAMA NI KWELI KWANINI WASIVIFADHI KATIKA UTARATIBU UNAOKUBALIKA KISHERIA! KAMA JIBU NI DIO BASI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE KWA KUSHINDWA KUTUMIA NJIA SAHIHI YA KUVITEKETEZA NA KUSABABISHA HOFU KWA WANANCHI.
2). KAMA KAMA LA, NI KWA VIPI WALIWEZA KUPATA VIUNGO VYA BINADAMU WENGI KIASI HIKI, NI KWA WATU WALIOPOTEA AMA KWA KUUWAWA JAMANI MBONA INATISHA SANA!
AMA USHIRIKINA? TUNAOMBA HUYO DEREVA ASEME ALIVITOA WAPI NA KAMA BADO KUNA VIUNGO VINGINE VIMEBAKIA HUKO ALIKOVITOA ALEZE KILA KITU ILI SHERIA IFUATE MKONDO WAKE.
MUNGU BABA TUNAOMBA UOKOE TAIFA LA TANZANIA.
mimi mwenzenu kwa miaka mingi nimekuwa najiuliza bila kupata jibu, nikiangalia luninga, ITV-Jiji letu, mara kwa mara unakuta tangazo la watu walio potea, kwa mwenzi ukifuatilia ni watu wengi, cha kushangaza sioni kama kuna mtu anae ona uzito wa hili swala,wanapotea wanaenda wapi? je huwa wanapatikanaga? na kwa nini watu wengi hivyo wanapotea, maana wiki haiishi lazima kuna mtu anatangazwa kapotea. Yani hadi naogopa, sasa hii ya leo ndio kali kuliko. Watanzania tunasubiri majibu tena yanayo jitosheleza.
ReplyDeleteHiyo hadi Gloves kuwepo itakuwa inatoka Hospital...Lkn hatakama ni hospital kwanini waende wakatupe Dampo? Je mtoto au binadamu uliye hai ukiona hivyo, wanatujengea nini? Watoto wetu wanawajengea nini? Si ndio watatuzoesha kuona maiti na watoto wetu wataona kama maiti na kuua ni kitu cha kawaida...
ReplyDeleteKwani hiyo imekuwa kuku atupwe jalalani...? Kwanini wasizike? Mbuzi mwenyewe au ng'ombe akifa hatupwi jalalani sembuse viungo vya binadamu!! Jamani kama ni Hospitali kwa hakika sheria ifuate mkondo...
Tunajua fika kuwa Mahospitali kama Muhimbili huwa wakati mwingien wanatumia Maiti zilizokuwa na wenyewe kujifundishia kwa Madoctor. ila kwanini watupe masalia Jalalani kama wanatupa taka za kawaida?
ReplyDeleteSi vizuri kabisaa...Wangezika basi kama wameshindwa kuchoma.
Tunaelekea wapi sasa maana huku tulipofika sipo ambapo tulitarajia na haya yote husababishwa na sisi wenyewe kwakweli inatisha sana imefikia wakati tutaogopa hata kwenda kwenye nyumba za ibada kuhofia maisha yetu
ReplyDelete" YARABI TOBA "
ReplyDeleteHii ni hatari sana!
ReplyDeleteKiukweli ni hatari sana mie sina la kusema
ReplyDeleteInasikitisha sana, tuwe watulivu tusubiri kupata ukiweli wa hizi maiti kutoka kwa serikali
ReplyDeleteCADAVA.....Hizi ni sampuli za maiti kwa ajili ya kujifunzia madaktari jamani...acheni kukuza mambo namna hii....kosa la chuo hicho ni kudspose vibaya...walitakiwa kuchoma maiti hizi.
ReplyDeleteBy KAFANABO/MNYAKYUSA PURE/DR
subhannallah
ReplyDeletehivi mi nahisi wanauza nyama ya watu
ReplyDeleteinavosemekana waliitupa baada ya kuona wakaguzi wanakuja but the issue is why waliogopa hadi wafike stage ya kutupa ovyo,...and why kama ni halali kutumia viungo hivyo kwa kufanyia practicals zao na kama ni legal waogope hadi kufanya hivi.....
ReplyDeleteNdio madaktari wanafunzi hutumia miili/maiti kujifunza umbo (anatomy) la mwili wa binadamu. Lakini baada ya kumaliza kuitumia miili, huchomwa kwa utaratibu maalum. Na wala watu wa nje (wasio katika fani) hawasitahili kilijua hili. Miili ya binadamu inastahili kuheshimiwa siku zote. Hicho ndicho nilichoambiwa na profesa wangu siku ya kwanza kabisa ya somo la anatomy. Huwezi kwenda kutupa mabaki ya mwili wa binadamu kwenye dampo. Inaonekana hivi vyuo vingine ni vyuo uchwara. Kama viongozi wake wanaweza kufanya hivyo, je ni aina gani ya madaktari wanazalisha? Maadili yako wapi? Sheria ichukuwe mkondo wake.
ReplyDeleteThese families donated their bodies to make us better doctors! I remember my cadaver like it was yesterday (trained 15 years ago)... I hold so much respect for her. I even wrote a poem at our last gathering ya kuwapa familia majivu take.... How could this institution be so inhuman... sasa hiko chuo kifutwe kabisa au walipe fidia yakutosha sio kwenda conference na kula padiem tu eti hawana pesa za kuchoma disgusting!
ReplyDeleteDu! Hii ni hari! Kwani hizo practical zipo mwaka huu tu?!! Hasbunaalah wa neema llwaakiiil.
ReplyDeleteDuuh,hii hatari kubwa sana,ubinaadamu upo wapi jamani? Nawaza sana!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteUbinaadamu upo wapi jamani? Watanzania wapi tunaenda? Nawaza saanaa!!!!!!!!!
ReplyDeleteHakika sheria ifuatwe na wahusika wakamatwe haijalishishi walitumia kwa mazoez au la!
ReplyDeleteYaaani. Eeee. Roho ya binadamu hao imekuwa ngumu hivi ? Wanasahau kuwa hicho kilikuwa sehemu ya mtu, pengine wengine wapo hai ? Na je we mhusika au wahusika ungefurahia kufanyiwa hiki kitendo ? Je ingekuwa ni kiungo cha familia yako ungesema haikugusi ? Wapi dhamira ? Na sasa sisi tuna simama na kusema mumefanya makosa. Hata madaktari wana ethical conduct ya ku dispose off viungo na mengineo. Hii inatuletea aibu kubwa sana kwenye jamii ya Afrika. Mbona mnaturudisha nyuma kimaadili hivi ? Nyie wachache kweli mumetuvunjia heshima kabisa. Mnatakiwa mujitokeze na mkiri mmekosa. Hiyo ni adhabu tosha. Naomba msibanie hii comment. Lazima wakuu wa idhara hii mtoe commentary, nyie mkinyamaza kimya tutayaona tena haya, ni aibu.
ReplyDeleteMungu upo wapi ? Amani imeshaondoka nchini, tamaa, ufisadi, ushirikana, ndiyo unatawala. Na ni wachache wanakosa hii nidhamu. Tusaidie Mungu.
Ni kweli inasikitisha kwani sio mazoe yetu watanzania kuona viungo vya binadamu hadharani kiasi hiki tena vikiwa vimetupwa jalalani. Lakini basi niseme nini nijuacho; Mimi nawalaumu sana wahusika waliamua kutupa viungo hivi vya binadamu katika hali hiyo, nijuavyo hawa ni Madaktari wetu wanafunzi ambao utumia miili ya binadamu katika moja ya masomo yao, na miili hiyo uipata ni katika zile maiti zisizo na wenyewe ambazo hukaa machuari kwa muda mrefu bila kupata ndugu zao, na hivyo ndizo zinazotumika katika kujifunza kwa Madaktari wetu.
ReplyDeleteSasa utaratibu ambao wameutumia hawa Menejimenti ya Hospitali (I......) ambapo si Madaktari tena kwenda kutupa kwa styre hile sio mzuri nadhani pamoja na kumaliza kuitumia miili hiyo walitakiwa kuchimba shimo kubwa na kufukia viungo hivyo na tena kwa kupata kibali cha Police ili kuepukana na lawama kama hizi ambazo zimesonga akili za watu pasi sababu yeyote wakati watu wanawaza nini leo wafanye katika maisha yao kisha wanakutana na habari hizi za kustua, hakika Uongozi wa Hospitali hiyo ya (I......) haikufanya vizuri.
Ikumbukwe Binadamu ni Binadamu tu haijalishi kafa kifo gani au alikuwa na tabia gani Maiti yake yapaswa kuheshimiwa! Hawa uongozi(Taifa lao) wanatudharau sana sisi waafrika, hivyo wachukuliwe hatua stahiki pux&*o#@)* hawa!
Mimi ni Mwanafunzi wa udaktari na ninakiri uwepo wa hizo practical vyuoni lakin nimesikitishwa sana na kitendo kilichofanywa na huo hicho..Ni wazi kwamba mtu hutokuwa daktari bila kujifunza pratical hizo mwaka wa kwanza,Lakin kuna maadili yanayotuongoza na mwili wa binadamu unatakiwa uheshimiwe...sidhana hata huyo mtupaji angependa ndugu yake atupwe kwa staili ile...hata kama hawana pesa basi wangewazika kwapamoja.....Hicho huo kipo after money na wahindi hawajaithamin miili kwa sababu ni ya watu weusi....CHUO KIWAJIBISHWE maana practical hizo ni siri mtu yeyote asiyehusika hastail kujua...
ReplyDelete