Na Andrew Chale, Bagamoyo
CHUO  cha Kilimo na Mifugo Kaole (Kaole College of agriculture (KCA), kesho Jumamosi Julai 12, kinatarajia kufanya mahafali yake ya pili chuoni hapo huku wahitimu  291, wakitarajiwa kutunukiwa vyeti mbalimbali.
Akizungumza mjini hapa,  principle wa chuo hicho,  Cuthbert Liwa alisema kuwa, tayari maandalizi yamekamilika na mahafali hayo yatafanyika kwenye viwanja vya chuo hiko.
“Jumla ya wahitimu 291, wanatarajiwa kuhitimu na kutunukiwa  vyeti vyao.   Kati ya hao, wahitimu 179, fani ya Kilimo na  wahitimu 112, kwa fani ya Ufugaji” alisema Liwa.
Aidha, alisema mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, anatarajiwa kuwa Dr. Masuruli wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Aidha, aliwaomba watu mbalimbali kujumuika kwa pamoja kwenye mahafali hayo, chuoni hapo, Kaole, Bagamoyo. (the college is located in South-East Bagamoyo 3.5 km from Bagamoyo township in the premises of Kaole Secondary school.  The centre is along the showers of the Indian Ocean).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...