Wajumbe wa Mkutano wa 45 wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya Ufunguzi wa Mkutano huo jana. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Ghalib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Ghalib Bilal akifungua Mkutano wa 45 wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC). Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 ambao ni Maspika, Wabunge na Maafisa wa Mabunge kutoka bara la Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Ghalib Bilal akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC). Kulia ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ndiye rais wa chama hicho. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 ambao ni Maspika, Wabunge na Maafisa wa Mabunge kutoka bara la Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...