CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimeipongeza klabu ya Simba kwa kufanya uchaguzi wa amani na kupata viongozi wake wapya watakaoingoza kwa miaka minne.

Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo, amema kuwa wana imani na uongozi huo mpya wa Rais Evans Aveva, Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Kamati yake ya utendaji.

“Sisi DRFA tunawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza klabu ya Simba kwa kipindi cha miaka minne, katika uchaguzi uliofanyika Juni 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Pilisi, Osterbay.

“Tunaamini kuwa wanachama waliowachagua viongozi hao wana imani nao na wataweza kuiongoza klabu hiyo kufikia mafanikio,” alisema Kassongo.

Alisema DRFA itakuwa tayari kufanya kazi na kushirikiana kwa karibu na uongozi huo katika kipindi chote cha uongozi wao na kuwataka kudumisha amani na utulivu ndani ya klabu hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Colin Fish, Jasmine Sudi, Said Tuli, Idd Kajuna na Ally Sum.
Imetolewa na Ofisa Habari wa DRFA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...