Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) Bw. Harbinder Singh Sethi (wa pili kulia) akimwonyesha kitu Fadha Gerald Kamina (wa pili kushoto) mara baada ya kukabidhi
hundi ya Shilingi milioni 14.5 kama msaada kwa jumuiya ya Kanisa la
Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, kusaidia ujenzi wa
kanisa hilo. Kushoto ni Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa
Kanisa hilo na kulia ni Rajiv Bhesania,
msaidizi wa Mwenyekiti mtendaji wa IPTL.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) Bw. Harbinder Singh Sethi (wa pili kulia) akikabidhi hundi ya shilingi
milioni 14.5 kwa Fadha Gerald Kamina (wa tatu kilia), kama msaada kwa jumuiya ya Kanisa la
Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, kusaidia ujenzi wa
kanisa hilo. Pamoja nao ni Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa
Kanisa hilo (wa tatu kushoto), Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL Bw.
Joseph Makandege (wa pili kushoto), Mwanasheria wa IPTL Melchisedeck
Lutema (wa kwanza kushoto) na wa kwanza kulia ni Rajiv Bhesania, msaidizi wa
Mwenyekiti mtendaji wa IPTL.
Katibu
na
Mwanasheria Mkuu wa IPTL Bw. Joseph Makandege (wa pili kushoto),
akimpongeza Fadha Gerald Kamina (wa tatu kilia), mara baada ya
Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL Bw. Harbinder
Singh Sethi (wa pili kulia) kukabidhi hundi
ya
shilingi milioni 14.5 kama msaada kwa jumuiya ya
Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam,
kusaidia
ujenzi wa kanisa hilo. Pamoja nao ni Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa
Kamati ya
Ujenzi wa Kanisa hilo (wa tatu
kushoto), Mwanasheria wa IPTL Melchisedeck Lutema (wa kwanza kushoto)
na
wa kwanza kulia ni Rajiv Bhesania, msaidizi wa Mwenyekiti mtendaji wa
IPTL.
========= ====== ======= =====
KAMPUNI ya ufuaji umeme ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imetoa msaada wa shilingi milioni
14.5 kwa jumuiya ya Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es
Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo.
Akizungumza katika hafla ya
kukabidhi hundi kwa jumuiya hiyo, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Bw. Harbinder
Singh Sethi alisema kuwa IPTL imetoa msaada huo ili kusaidia katika ujenzi wa
Kanisa hiyo ya Mtakatifu Petro.
“Hizi
milioni 14.5 tulizotoa kwa Kanisa la Mtakatifu Petro, ni sehemu ya utekelezaji
wa mpango wetu wa kuwezesha miradi mbali mbali za kijamii ambazo zinagusa
maisha ya watu wengi. Tuna imani kwamba kwa kuchangia fedha hizi zitasaidia
kusukuma mbele ujenzi wa kanisa hili ili liweze kukamilika mapema na kutumika
kwa ajili ya ibada.
“Jitihada
hizi ni moja kati ya mkakati wetu wa utekelezaji wa mpango wetu wa kutumia
sehemu ya faida tunayopata kutokana na shuguli zetu, kwa kuiwezesha jamii
katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo kiuchumi. Misaada kama haya
hayalengi tu kusaidia vijana wa kitanzania kuendelea kiuchumi lakini pia
misaada kwa taasisi za kidini itasaidia katika kujenga jamii inayo mcha Mungu
na hivyo taifa kuwa katika mazingia mazuri ya kupiga hatua kubwa kimaendeleo,”
alisema Sethi.
Bw.
Sethi alisema kuwa kampuni yake ina mpango madhubuti unaolenga kusaidia
mashule, makanisa, misikiti na mashirika mengine yasiyoyakibiashara yanayofanyakazi
ili kuwawezesha vijana kuwa wachangiaji wakubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi
Tanzania.
Naye
Katibu na Mshauri Mkuu wa IPTL, Bw. Joseph Makandege alisema kuwa IPTL ikiwa na
mpango wake wa kuunga mkono jitihada mbali mbali za kimaendeleo na kijamii, itaendelea
kushirikiana na jumuiya mbali mbali ili kwa pamoja kuona kwamba fursa mbali
mbali za kiuchumi zinazojitokeza zinapewa msukumo kwa ajili ya maendeleo ya
jamii kwa ujumla.
“Kama
IPTL, tumeona kuwa ni jukumu letu kuisaidia jamii inayotuzunguka. Nina imani
mchango wetu kwa Jumuiya ya Mtakatifu Petro leo hii utasaidia kuongezea nguvu
ujenzi wa Kanisa unaoendelea. Lengo letu ni kuona kwamba tunachangia maendeleo
ya kiuchumi lakini pia bila kusahau jamii yetu inayotuzunguka zikiwepo jumuiya
mbali mbali za kidini,” alisema Bw. Makandege.
Kwa
upande wake, Bi. Rose Rupia, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo,
aliishukuru IPTL kwa msaada wake na kusema kuwa fedha iliyotolewa itasaidia kwa
kiasi kikubwa kusukuma mbele ujenzi wa kanisa hilo ambao bajeti yake ni zaidi
ya shilingi milioni 600.
“Naishukuru
IPTL kwa kuona umuhimu wa kukubali ombi letu na kuja kutuunga mkono katika
jitihada za ujenzi wa kanisa letu. Fedha hizi zitasaidia kusukuma mbele zaidi
ujenzi wa kanisa letu, huu ni mfano mzuri wa kuigwa na makampuni mengine na
watu binafsi,” alisema Bi. Rupia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...