Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa.
WATEJA wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu wanatarajiwa kuchezeshewa droo maalum itakayotoa zawadi mbalimbai ikiwemo pikipiki.
Katika droo hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na atakabidhi zawadi kwa wateja mbalimbali watakaojishindia zawadi hizo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer alieleza kuwa, droo hiyo ni maalum kwa ajili ya wateja wote waliopata kutembelea banda hilo tokea siku ya kwanza na kujiorodhesha majina yao
Fatema alisema MeTL Group imeamua kutoa zawadi hizo kama shukrani na kujitangaza zaidi kwa wateja na wananchi waliopata kutembelea na kununua bidhaa za MeTL Group.
“Kwa ubora wa bidhaa zetu za MeTL Group, kama inavyojulikana, ‘The People’s Brand’, kwa droo hii wateja wetu watafurahia kwa zawadi hizo nono” alisema Fatema.
Katika droo hiyo, zawadi kuu ni pamoja na Pikipiki, zawadi za khanga, vitenge, mashuka, sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupikia, unga na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Aidha, MeTL Group imetambulisha rasmi vinywaji vyake vipya kwenye maonyesho hayo ya Saba Saba, ikiwemo kinywaji kinachopendwa na wengi kwenye maonyesho hayo, MO Cola, MO Portello na MO Malt. Vingine ni MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...