Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba,Yahya Khamis Hamad akizungumza na Wanahabari mapema leo mchana katika ofisi ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar,kuhusiana na maoni na ushauri wa kikao cha kamati ya Mashauriano ya Bunge maalum la katiba kilichofanyika jana julai,24,2004 katika Ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar.Mh. Yahya alisoma taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Samuel Sitta.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba,Yahya Khamis Hamad,katika mkutano uliofanyika mapema leo katika ofisi ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar.
Haya ni masihara na kupoteza hela za wananchi. Rasimu ya katiba ipelekwe moja kwa moja kwa wananchi; wananchi wataamua kuikubali au kuikataa. Cha msingi tu tuwe na tume huru ya kusimamia zoezi hilo
ReplyDeleteWazimu ncha Saba haya endeleeni na USANII wenu Bungeni tuone kama hiyo inayoitwa Katiba kama itapita kwa Wananchi
ReplyDeleteTatizo akina Kaisari wanafikiri wao ndo Tanzania na Tanzania ndo wao. Kila waamualo wao waspingwe! Haya wakaandike katiba yao pale bunjeni na sisi wananchi tuaandika ya kwetu huku mtaani.
ReplyDelete