Michael Jackson alipoitembelea Tanzania Februari 1992. Alitua uwanja wa ndege wa Dar kwa ndege yake mwenyewe  akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Benzi s iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, ambapo sasa ni  Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam. 
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani kama Mfalme wa Pop hadi anakufa mwaka 2009, alifika nchini akiwa balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Hassan Diria (juu kushoto). 
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na Rais Ali Hassan Mwinyi. Kesho yake alitembelea shule maalum ya watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo iliyopo Sinza. 
Ndege yake iliyokuwa na watu takriban 60 ilishindwa kwenda mbugani Ngorongoro alikotaka kwenda. Na yeye alikuwa hawezimkupanda ndege ndogo, hivyo akaishia Dar es salaam. 
Sehemu  ingine aliyotembelea na kuacha gumzo ni jumba la sinema la Empire mtaa wa Azikiwe ambako aliingia katika duka la kukodi mikanda ya sinema. Naye alibeba mikanda kama 10 hivi ya vikatuni, ikiwemo ya Tom and Jerry.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2014

    One word michuzi, ASANTE

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2014

    michael alipotua airport alitaraji kupanda rolls royce ambalo halikuwepo. hivyo badala yake alipanga ktk nissan patrol ambapo alikaa kiti cha nyuma pamoja na katoto kamoja ka kidhungu. Hakutaka kupanda benz lililokuwepo pale

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2014

    Hivi mlimualika wa kazi gani wakati aliukana uafrika na kujibadili kuwa mzungu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...