Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza 6 Oktoba kuwa ni tarehe ya kuanza kwa mafunzo ya stashahada ya ualimu wa shule za msingi (Ordinary Diploma in Primary Education (ODPE)) katika vyuo teule vya majaribio na Stashahada maalumu ya Ualimu wa Sekondari kwa waliomaliza kidato cha nne (Hisabati na Sayansi) itakayoendeshwa katika chuo kikuu cha Dodoma.

Zoezi la uombaji wa mafunzo hayo kwa mwaka 2014/15 lilianza rasmi tarehe 23 June 2014 na litakoma 31 Agosti 2014 na mafunzo yataendeshwa katika vyuo teule vilivyoteuliwa na Baraza (NACTE) ambavyo vitaendesha mafunzo chini ya uangalizi wa karibu wa Baraza hilo, Taasisi ya Elimu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Primus Nkwera amesema waombaji wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu wa uombaji ambao ni kupitia njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System - CAS) inayopatikana kwenye tovuti ya CAS inayopatikana www.cas.ac.tz au Baraza www.nacte.go.tz na kwamba Baraza halitomtambua mwombaji yeyote atakayeomba kinyume na utaratibu uliowekwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...