Waziri Mkuu Mizengo Pinda, (Kushoto), akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani, wa PSPF, Goddfrey Ngonyani, wakati alipotembelea banda la mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Mahusiano na Masoko, Costantina Martin.
Mkazi huyu wa jijini Dar es Salaam, akipatiwa huduma na mtafiti mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Maagi Thomas, kwenye banda la Mfuko huo lililoko kwenye jengo la wizara ya fedha kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, Jumatano Julai 2, 2014.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Kushoto), akizungumza na Waandishi wa habari kutoka Uingereza, Oliver Moss(Katikati), na Carla de Campos, walipotembelea banda la PSPF kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, Jumatato Julai 2, 2014.
Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani, Goddfrey Ngonyani,watatu kushoto), Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Costantina Martin, (Watatu kulia), kwenye banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, Jumatano, Julai 2, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...