Mbunge  wa Viti maalum(CCM) mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiangalia bweni la shule hiyo ya Irkisongo wilayani Monduli lililoteketezwa na moto 
 Mapacha wanaoishi Wakaazi wa New York Marekani Joy na Jane wakimkabidhi mkuu wa shule hiyo mama Nyange sehemu ya msaada wao wa kilo zaidi ya kumi za misumari
  
Mjumbe wa kamati ya siasa(CCM) wilaya Monduli, Paulina Ngoyai(Mama Kalaine) akikabidhi msaada wake wa mifuko mitano ya sementi kwa shule hiyo

 Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha(CCM) Namelok Sokoine akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Irkisongo wilayani Monduli Happiness Nyange msaada wake wa shilingi millioni moja kufuatia kuungua kwa mabweni ya shule hiyo

Mwakilishi wa kiwanda chaTanfoam cha jijini Arusha Sajid Ibrahim(kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi millioni 3 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Irkisongo Wilayani Monduli Happness Nyange(kushoto), kufuatia mabweni ya shule hiyo kuteketea kwa moto hapo jana.Msaada huo unatokana na harambee ya papo kwa papo aliyoifanya mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akitumia simu yake ya kiganjani. Wadau kadhaa wa elimu wamejitokeza kusaidia ambapo mbunge wa Arusha Viti maalum Namelok Sokoine amechangia shilingi millioni moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...