Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio akisalimiana na mmoja
wa wafanyakazi wa Mfuko huo wakati alipotembelea Banda laa PPF kujionea
utendaji kazi wa Wafanyakazi wake katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja vya
Mwl Nyerere.
Mkurugenzi
Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio akiteta jambo na
wafanyakazi wa PPF wakati alipotembelea Banda la PPF kujionea utendaji
kazi wa Wafanyakazi wake. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Bi
Lulu Mengele na Katikati ni Mbaruku.
Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna
Shayo akimuhudumia mteja aliyefika katika Banda la PPF kwaajili ya
kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo wa
PPF.
Afisa
Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel (kushoto) akirufahia
jambo na mmoja wa wateja wa PPF aliyefika katika banda la PPF kwenye
Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja hivyo
vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza kwa makini mmoja wa mteja
aliyefika katika banda la PPF kwaajili ya kujiunga na Mfuko huo wa
Pensheni wa PPF katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika.
Afisa
Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa PPF, Mohamed Siaga akitoa maelekezo kwa
mteja aliyefika kwenye dawati lake kwaajili ya kupata maelekezo juu ya
huduma mbalimbali za mfuko wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar Es Salaam.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...