GAZUKO AKIWA KWENYE POZI
Gazuko ni kijana pekee ambaye anafanya muziki wa injili kwa style ya Hip hop na ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa injili wanaoiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye Tuzo za Africa Gospel Music Awards kwa kifupi zinajulikana kama (AGMA) ambapo kwa hapa Tanzania mwaka huu wameingia waimbaji kama Rose Mhando,Christina Shusho pamoja na Gazuko...
Gazuko ameomba watanzania na wasio watanzania waweze kumpigia kura kwa wingi ili aweze kuchukua hiyo tuzo ya AGMA ambayo kwake ni ndoto yake kuipata Gazuko kwenye tuzo hizo yupo kwenye category ya Afro Rap Artiste Of The Year ndani ya category hiyo kuna ushindani wa wanahip hop 15 kutoka nchi mbali mbali za  Africa na Ulaya hivyo Gazuko anaomba kura yako ili aweze kutimiza ndoto yake na pia kuliletea Taifa letu heshima.
Jinsi ya kupiga kura ingia kwenye website ya http://www.africagospelawards.com/vote.html halafu nenda mpaka kwenye category ya AFRO RAP ARTISTE OF THE YEAR utaliona jina la Gazuko (Tanzania) hapo utaweza kumpigia kura kwa kuweka nukta nyuma ya jina lake na ukimaliza unatelemka hadi mwisho wa category unabonyeza neno "VOTE" na kwa kufanya hivyo utakuwa umewezesha Taifa letu kujipatia ushindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...