Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari. 
Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wahariri wa vyombo vya habariMkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada katika mkutano huo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada katika mkutano huo.Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.[/caption] MTANDAO wa Wanawake na Katiba umevitaka vyombo vya habari kuacha kuyumbushwa na upepo wa kisiasa katika suala zima la kupigania mambo ya msingi kwa jamii ambayo yanaitaji kuingizwa kwenye Katiba mpya kwenye mchakato unaoendelea hivi sasa wa kuandika katiba mpya. 

 Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wajumbe wanaounda mtandao huo jijini Dar es Salaam walipokuwa wakizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuelezea msimamo wa wajumbe hao kwenye mchakato wa uandikaji katiba mpya. 
 Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu aliviomba vyombo vya habari kuwaunga mkono wanamtandao hao ambao pamoja na mambo mengine wamejipanga kupigania kero za wananchi kuhakikisha zinapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya hivyo kuwataka wanahabari kuwaunga mkono. 
 Alisema vyombo vya habari visikubali kupelekeshwa na wanasiasa kwa kupaza sauti kwenye maslahi ya wanasiasa zaidi na kushindwa kujadili masuala ya msingi ya jamii, ambayo endapo yatapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya wananufaika ni wananchi wote tofauti na masuala ya utawala (madaraka). 
 "Waandishi wa habari msikubali kuchezeshwa ngoma za wanasiasa, ambao mara zote wanapigania maslahi yao kiutawala...tupiganie maslahi ya jamii, jamii inaitaji kuona huduma bora za afya, elimu na mgawanyo sawa wa rasilimali," alisema Dk. Semakafu. 
 Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari alisema vyombo vya habari vina nguvu za kipekee katika kuleta mabadiliko kwenye jamii na mamlaka hivyo kuwaomba watumie fursa hiyo ipasavyo katika kupigania maslahi ya umma. 
 "...Hivyo vyombo vya habari, kama msingi wa kupatikana kwa taarifa yoyote, na kuongoza katika ushawishi vina sehemu muhimu sana katika kuongoza kuleta mabadiliko yawe ya sera, tabia au utamaduni," alisema Bi. Msoka ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba. 
 Hata hivyo alivitaka vyombo vya habari kuwaunga mkono wanawake kwani licha ya kuwa na mchango mkubwa katika jamii wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kusahaulika kwenye fursa anuai zilizopo. 
"...Wanawake ni asilimia 80 ya nguvu kazi vijijini na ni asilimia 60 ya wazalishaji wakuu wa chakula...lakini tunachangamoto nyingi," alisema Bi. Msoka. Mtandao wa Wanawake na Katiba ni muunganiko wa asasi za kijamii na kitaaluma zipatazo hamsini zilizoungana kudai katiba inayozingatia masuala ya kijinsia na inayotokana na mchakato ulioshirikisha sauti za makundi yote. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...