Makamu wa Pili wa
Raisi, Balozi Seif Idd, akimkabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza katika sekta ya mifuko ya Hifadhi ya
Jamii, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Crescentius Magori wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa
(DITF), katika Vinwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mh. Balozi Ally Seif akipata ufafanuzi kutoka kwa Meneja Miradi Mhandisi John Msemo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhusu Mradi wa DEGE ECO VILLAGE. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya kimataifa ya 38 (Sabasaba) katika viwanja vya Mwalimu Jilius Nyerere. Wa pili kulia ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii-NSSF.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Janeth Mbene akipata maelezo kuhusu mpango wa uchangiaji wa wakulima kwa wanachama walio katika sekta isiyo rasmi kutoka kwa Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma Kwa Wateja Mrs Eunice Chiume wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya 38 ya kimataifa ya Sabasaba. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Crescentius Magori.
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu mradi wa DEGE ECO VILLAGE kutoka kwa Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi P. J. Msemo alopotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Waziri wa viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda.
Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifurahia tuzo za ushindi wa jumla katika sekta ya Hifadhi ya Jamii na Bima
katika maonyesho ya kimataifa ya 38 (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...