KLABU ya yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba kwa ajili ya
wachezaji wake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika mkutano maalum na wachezaji hao Mkurugenzi
wa uendeshaji NSSF, Crescentius Magori amewaambia wachezaji hao kuwa "kijana mjanja mjini ni yule ambaye ana miliki nyumba ama ardhi kuliko
magari" huku akiwahamasisha wachezaji wa Yanga kuchangamkia ununuzi wa
nyumba hizo ambazo ziko katika mradi wa makao mapya katika kijiji cha
Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo
ambazo zimejengwa kisasa zaidi hivyo ningependa kuwashauri pindi
mnapopata fedha zenu za mikataba mkitoa kiasi ili kuweza kuwa kati ya
wamiliki wa nyumba hizo” alisema Magori.
“Endapo utaweza kumudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 taslimu na
kulipa kwa miezi mitatu mfululizo unapewa NSSF wanamupa funguo na
kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi hadi kwa miaka 15 unakuwa
mmiliki halali wa nyumba hiyo”alisema Magori.
Aidha aliongeza kwa kuwaambia wachezaji hao kwamba endapo utakufa
ndugu anaweza kurithi nyumba hiyo.
Huku akiwasisitiza wachezaji ambao bado hawajajiunga na NSSF kufanya
hivyo mara moja ili waweze kujivunia matunda ya uchezaji wa mpira hapo
baadaye.
Wakati huohuo Katibu wa Yanga Beno Njovu aliwaambia waandishi wa
habari kwamba hayo ni mawazo ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji
ambaye alizungumza na Mkurugenzi wa NSSF Ramadhan Dau ambapo wote kwa
pamoja wameamua kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na
mali zao za kudumu hadi uzeeni.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Yanga wakati wa mkutano wao wa kuzungumzia umuhimu kwa wachezaji hao kumiliki nyumba zao,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akifafanua jambo mbele ya wachezaji wa timu ya Yanga na viongozi wa timu hiyo (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Timu ya Yanga,Beno Njovu akieleza nia ya Timu yake ya kutaka kuwawezesha wachezaji wao waweze kuwa na Nyumba zao wenyewe.
Watendaji wakuu wa NSSF
Sehemu ya Uongozi wa Timu ya Yanga chini ya Kocha Mkuu,Marcio Maximo.
Wachezaji wa Yanga wakipitia vipeperushi walivyopewa juu mradi wa nyumba za bei nafuu za NSSF.
Baadhi ya Wachezaji wa Yanga wakifatilia kwa makini maelezo waliyokuwa wakipewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...