Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Dkt. Parseko V. Ole Kone kuomboleza kifo cha aliyepata kuwa Naibu Waziri, Mbunge na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mheshimiwa Alhaji Mahami Rajab Kundya, aliyefariki dunia jana, Jumapili, Julai 27, 2014 mjini Zanzibar.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa taifa limempoteza Mzee Kundya katika kipindi ambacho ushauri wake ulikuwa unahitajika sana na kuwa Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa mchango wake katika nafasi zote alizozishikilia za Serikali, za Chama cha Mapinduzi na za kidini.

Naungana nawe na wana-Singida wote katika kuomboleza kifo cha Mzee Kundya.Tumepoteza kiongozi ambaye mchango wake utaendelea kukumbukwa na sisi sote. Kupitia kwako, natuma pia salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu. Niko nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa na naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Kundya,” amesema Rais Kikwete.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

28 Julai,2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...