Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na Mkewe Princess Akishino  walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mkurugenzi wa Idara ya Asia Bw. Mbelwa Kairuki kwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazunzumzo na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014. walioketi kulia ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Balozi wa Tanzaia nchini Japan Mhe Salome Sijaona
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa historia ya Ikulu  Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino  mbele ya lango kuu ya Ikulu hiyo ya Dar es salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatembeza Ikulu Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe  Princess Akishino walipomtembelea jijini Dar es salaam leo July 3, 2014. Wengine ni WaZiri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe (wa pili kulia) , Naibu WaZiri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt Mahadhi Juma Maalim, balozi wa Tanzania nchini japan Mhe Salome Sijaona (kushoto) na balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe Masaki Okada (wa pili kushoto).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha Simba waliotengenezwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Alhamisi, Julai 3, 2014, amemkaribisha Ikulu, Dar Es Salaam, Mwana wa Mfalme wa Japan, Prince Akishino pamoja na mkewe Princess Akishino.
Mwana Mfamle huyo ambaye anatembelea Tanzania, amewasili Ikulu kiasi cha saa nne asubuhi na kufanya mazungumzo ya zaidi ya nusu saa na Mheshimiwa Rais Kikwete.
Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete amesema kuwa Japan ni mshirika mkubwa na muhimu sana wa maendeleo ya Tanzania. “Tunathamini sana mchango wenu katika maendeleo ya Tanzania na tunaendelea kuwashukuru sana. Ukizunguka nchini mwetu utaona kwa macho yako miradi mingi na mikubwa ambayo imejengwa ama inajengwa kwa msaada wa Japan.”
Rais kikwete ameongeza: “Pamoja na ushirikiano huu. Bado tunaamini kuwa Japan inaweza kusaidia zaidi Tanzania hasa kwa kushawishi makampuni yake kuwekeza katika sekta binafsi. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam, magari tisa kati ya 10 ni ya Kijapan. Ukiingia katika maduka ya vyombo vya elektroniki  - televisheni, kompyuta, camera, karibu kila kitu kinatoka Japan. Hali hii inathibitisha kuwa bidhaa vya Japan zina soko kubwa na zinaweza kuzalishwa hata hapa nchini na makampuni binafsi.”
Rais Kikwete pia ameitaka Japan kuangalia jinsi gani inavyoweza kusaidia ongezeko la watalii kutoka Japan kuja kutembelea Tanzania kwa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka huko hadi Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
“Wataalii wengi kutoka Japan wanashindwa kuja Afrika kwa sababu hakuna shirika hata moja la ndege la Japan ambalo lina safari za kuja Afrika, hata Afrika Kusini hakuna. Hii ndiyo maana hatuoni watalii wengine kutoka nchi za kusini mashariki mwa Bara la Asia kutembelea vivutio vyetu vya utalii,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Kama kuna jambo halionekani sasa katika uhusiano wa Tanzania na Japan ni uwekezaji katika sekta binafsi. Hili ndilo jambo tunaloliomba.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
3 Julai, 2014


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...