Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, Mhe. Prof. G.L. Peiris walipokutana mjini Colombo, Sri  Lanka wakati wa ziara ya Mhe. Membe nchini humo hivi karibuni. Wakati wa ziara hiyo  Mhe. Membe kwa niaba ya Serikali ya Tanzania alisaini mikataba mitatu ikiwemo ule wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Sri Lanka, Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya Siasa na Mkataba wa Makubaliano katika Maendeleo na Utafiti wa Kilimo endelevu cha Minazi.
Mhe. Membe na Ujumbe aliofuatana nao (kushoto) wakati wa mazungumzo na Mhe. Peiris na Ujumbe wake (kulia)
Mhe. Membe na Mhe. Peiris wakisaini Mkataba wa kuanzisha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Sri Lanka.
Mhe. Membe na Mhe. Peiris wakibadilishana Mkataba mara baada ya kuusaini.
Mhe. Membe na Waziri wa Kilimo wa Sri Lanka wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Maendeleo na Utafiti wa Kilimo endelevu cha Minazi.
Mhe. Membe na Mhe. Prof. Peiris wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano waliyokubaliana.
Wajumbe kutoka Tanzania na Sri Lanka pamoja na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mhe. Membe na Mhe. Peiris (hawapo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...