Mkurugenzi
wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele
ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari,wadau na wasanii wa
filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16,
2014 kutoka kwao na kuelekea kampuni ya No Fake Zone (NFZ) ambao ndiyo
wanaanza kumsimamia msanii huyo pamoja na kazi zake.Linah pia alizindua
video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo OLe Themba.
MKurugenzi wa Kampuni ya NO FAKE ZONE,Abby akizungumza jambo mbele
ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari,wadau na wasanii wa
filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16,
2014 ambaye anahamia hiyo,itakayokuwa ikisimamia kazi zake za msanii
huyo.Linah pia alizindua video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo
OLe Themba.
Msanii
Linah akizungumza na kutoa shukurani mbalimbali kwa wadau wa muziki
walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kumpa sapoti katika anga ya
muziki wa kizazi kipya.
Mkurugenzi
wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akimkabidhi cheti cha
heshima msanii wa kizazi kipya,Mwasiti kwa kuwa msanii mwenye nidhamu
kubwa kutoka chuo cha kipaji cha THT kwa muda mrefu.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa video mya ya Linah iitwayo OLe Themba
Msanii
Linah akiwa amepozi kwenye bango lake linaloelezea ujio wa video yake
mpya ya Ole Themba pamoja na jina la kampuni anayohamia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...