Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora leo yafanya hafla fupi ya kuagana na mtaalamu wa masuala ya ulinzi na haki za watoto wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Bi Rachel Harvey ambaye anahamia nchini Nigeria anakokwenda kuwa mkuu wa Kitengo cha kutetea na ulinzi wa haki za watoto.

Bi Rachel amekuwa akifanya kazi karibu na Tume katika kipindi chote cha miaka mine (4) aliyokuwa nchini, baadhi ya kazi alizofanya akiwa na Tume ni pamoja na kuratibu kazi mbalimbali kuhusiana na masuala ya haki za watoto katika mkinzano na Sheria; Mwaka 2011 Bi Rachel alishirikiana na ujumbe wa Tume kukagua magereza, vituo vya polisi, mahabusu ya watoto na shule ya maadilisho katika mikoa ya Mbeya na Iringa.

Bi. Rachel atakumbukwa sana kwa mchango wake mkubwa aliokuwa nao katika kuboresha haki za watoto nchini. Alishiriki kikamilifu katika kuandaa kanuni za sheria ya mtoto, kuwajengea uwezo wadau juu ya sheria ya mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na kushiriki katika maandalizi ya mkakati wa miaka mitano wa Haki za watoto unaoratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Tume ya Haki za Binadamu itaendelea kuenzi juhudi za Rachel za kuunganisha taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki za watoto katika mkinzano na sheria ambapo nyenzo mbalimbali za ufuatiliaji ziliandaliwa katika kufuatilia watoto katika vizuizi mbalimbali nchini.
Mheshimiwa Kamishna Ali Hassan Rajab na Katibu Mtendaji Bi. Mary Massay wakimkabidhi Rachel zawadi ndogo iliyoandaliwa kwa ajili yake.
Wakurugenzi na maafisa walioshiriki hafla hii wakisikiliza kwa makini.
Katibu Mtendaji Bi. Mary Massay akitoa neno la shukrani kwa Rachel
Kamishna wa na Kaimu mwenyekiti wa Tume Tume Mhe Ali Rajabu akisoma hotuba fupi kwenye sherehe yakuagana na Rachael Haevery, kulia kwake ni Rachael Harvey.
Picha ya pamoja kati ya wajumbe wa Tume na Bi Rachel.
Picha ya pamoja kati ya wajumbe wa Tume na Bi Rachel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...