Baada ya kuridhishwa na matumizi mazuri na mafanikio makubwa ya Maktaba yao ya kwanza waliyoifungua mwaka 2009 katika kijiji cha Ngongongare Mkoani Arusha,  Taasisis isiyo ya kiserikali ya The Crawford Smith Foundation yenye makazi yake nchini Marekani na ambayo ndiyo inayosimamia mradi wa uanzishwa na uendeshaji wa Maktaba hususani katika maeneo ya vijijini, sasa inakusudia kujenga maktaba nyingine sita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
 Maktaba hiyo ya kwanza na ya aina yake na ambayo imepewa jina la Jifundishe Free Library, si tu inatoa huduma za vitabu vya kiada na ziada kwa watumiaji ambao ni kuanzia wale wa shule za awali, msingi, sekondari na hata vyuo vikuu, bali pia imekuwa kituo ambacho kinawasaidia wanawake na vijana kujifunza stadi mbalimbali zikiwamo za ujasiliamali, vyama ya kuweka na kukopa, huduma za kinga ya afya, huduma za internet na mafunzo ya ziada ambayo yamekuwa yakitolewa na wataalamu wa kujitolea kutoka nje na ndani ya Tanzania. 
 Hayo yameelezwa na Viongozi wakuu wa Taasisi hiyo ya The Crasford Smith Foundation wakati walipofika na kufanya Mazungumzo na Balozi Tuvako Manongi Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. 
 Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Steven Smith aliyekuwa amefuatana na Mke wake Bibi. Judithi Smith amesema kuwa mwitikio mkubwa na matumizi sahihi na endelevu vya Jifundishe Free Library na matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani yao, kumewafanya watambue ni kwa kiasi gani huduma hiyo muhimu inahitaji kusambazwa katika maeneo mengine hasa ya vijijini. Lengo likiwa ni kuwafikia na kuwapatia huduma hiyo wasio kuwa na uwezo wa kuipata kwa urahisi. 
 Mradi huo wa Maktaba licha ya kutoa huduma mbalimbali, lakini umekwenda mbali zaidi kwa kutoa ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi wanne hadi sasa. baadhi ya wanafunzi hao wamerudi na kutoa mchango wao katika Maktaba hiyo na jumuiya inayoizunguka. 
 Baadhi ya maeneo ambako wanakusudia kupelea huduma hiyo muhimu ya maktaba ni Kisarawe , Chunya , Iringa, Morogoro na Kilimanjaro. 
 Aidha wakuu hao wameeleza kuridhidhwa kwao na Ushirikiano wanaoupata kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, baadhi ya Makampuni ambayo yameonyesha nia ya kushirikia na Taasisi hiyo katika utoaji wa huduma hiyo, na vilevile mwamko na moyo wakujitolea wa watanzania katika maeneo wanayokusudia kuanzisha maktaba hizo. 
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Balozi Manongi aliishukuru Taasisi hiyo kwa mchango wake mkubwa na ambao umeonyesha mafanikio na mabadiliko makubwa kwa jamii inayohudumiwa. 
Akasema Tanzania inatambua umuhimu wa maktaba katika mustakabali mzima wa elimu na mafunzo na kwamba mchango wa taasisi zisizo za kiserikali unakaribishwa sana.
 Kutoka kushoto ni  Bw. Steven Smith,  Bi Ann Hanin, Mhe.  Balozi   Tuvako Manongi na Bibi Judith Smith

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...