mwenyekit
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.

Na Hillary Shoo, SINGIDA.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.

Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa za mitaani.
kinyeto
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akizungumza kwenye shule ya sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
“Nataka niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo, haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu wanajipitishapitisha wakitukana.” Alisema Hanje kwa hasira.

Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
“Mimi inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani ya Chama Willaya hii.” Alisema Hanje kwa kujiamini.
diwani
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Lazaro Nyalandu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...