Ofisa habari wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Grace Msovela na baadhi ya viongozi wengine wa halmashauri ya mji huo wakikagua vyeti kabla ya kuvikabidhi kwa washindi wa mabanda ya idara mbalimbali za mji huo kwenye hitimisho la wiki ya Serikali za Mitaa ambapo kauli mbiu yake ni Katiba mpya izingatie kuwa Serikali za Mitaa ni msingi wa maendeleo endelevu:Mwananchi shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Andrew Ombay (Baba Salawo) akizungumza jana kwenye kilele cha wiki ya Serikali za Mitaa, ambapo alisema utawala wa Serikali za Mitaa ulianza kabla ya ukoloni ambapo machifu walikuwa wanaongoza utawala huo.
Baadhi ya watumishi wa idara ya afya wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, wakiwaonyesha wananchi waliotembelea banda lao, namna wanavyotoa huduma za afya kwa mama mjamzito, katika kilele cha wiki ya Serikali za Mitaa jana kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
Kaimu Mkurugenzi wa mji wa Babati, Mathias Mugorozi akizungumza jana kwenye kilele cha wiki ya Serikali za mitaa, ambapo alisema mji huo unatarajiwa kujenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita kumi ambapo mji huo utazidi kupendeza, katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Andrwe Ombay na Ofisa Elimu Sekondari, Nivoneia Levery.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...