MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera Bi. Zipora Pangani ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel kwa kufungua duka kubwa, ambalo litatoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo kutuma na kutoa fedha ya (AIRTEL MONEY).

Akifungua duka hilo lililopo eneo la Mtaa wa Kawawa Mjini Bukoba, alisema litakuwani chachu ya maendeleo, kwa wakazi wa mkoani Kagera ambapo litarahisisha huduma kwa wananachi.

“Ufunguzi wa hili duka hapa kwetu litakuwa ni chachu ya maendeleo kwa wateja wa Air tel na wananchi kwa ujumla hasa kwenye matumizi ya huu mfumo wa air tell money” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa kagera na maeneo jirani kuhakikisha kwamba wanaitumia hiyo fursa vizuri ili kuhakikisha wanakuza uchumi wao katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania alisema ufunguzi wa duka hilo ni mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine nchi nzima ili kutoa huduma bora kwa wateja wake.

“ Kampuni yetu ya Airtel tuna mpango madhubuti wakuhakikisha maduka yetu yote yanakuwa na mwonekano sawa na kutoa huduma bora zenye kiwango cha hali ya juu kwa wateja wetu kutokana na mahitaji yao” Aliongeza

“ Dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendeana na kasi ya uhutaji kwa wateja wetu kwenye mawasiliano ya kisasa na teknolojia, ya hali ya juu” Alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa Upande wao wateja wa kampuni hiyo waliojitambulisha kwa majina ya Joseph Kamuntu na Eradius Ernest wakizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa duka hilo waliishikuru kampuni hiyo na kwa kuwasogezea huduma hiyo.

“ Tunawashukuru sana hawa watu jamani yaani binafsi nimefurahi sana kupata hii huduma karibu sasa hivi wamefungua nimeingia mara moja nimehudumiwa ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine,” Alisema Kamuntu.

Aliyaomba Mkampuni mengine ya simu kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa huduma bora ambazo zinamjali mteja ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa kwa pande zote.

Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel hadi sasa imefungua maduka 11 hapa nchini katika mikoa ya Dar es salaam, Kagera, Dodoma ,Morogoro, Mtwara, Mbeya, lengo likiw ani kuhakikisha wananachi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, anaefuata ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akiongea na wananchi na wanahabari waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) pamoja na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (kushoto) akimuelezwa jambo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani mara baada ya ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani (kati) akikata keki maalum iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja Bukoba kwaajili ya hafla ya kusheherekea ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani hapo. Wakwanza kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Bi Adriana Lyamba na meneja wa duka hilo bukoba bi Anna Mapunda, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...