Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu, Bi. Nikki Clarke akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, katika Jengo lao lililopo Mikocheni jana jioni. Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,  Bw. Ali Saleh.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bw. Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, Bw. Hassan Mhelela (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu yake.
Taswira za Studio za BBC jijini Dar es salaam.
Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar es salaam.
Picha na zote na Othman Michuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...