Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB),Bwa.Viju Cherian akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Mapema leo ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano Serena Hotel jijini Dar kuhusiana na ripoti ya nusu mwaka wa 2014 kuhusu utendaji wa benki hiyo kwa ongezeko kubwa la faida kabla yakodi (profit before Tax (PBT) ya sh.billioni 10.3 ikiwa ni  asilimia 38 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2013 sambamba na mafanikio makubwa iliyoyapata benki hiyo.

Bwa.Viju alisema kuwa mwaka 2014 unatoa matumaini ya kuwa mwaka mwingine mzuri kibiashara kwa DTB,alisema kuwa mafanikio yalipatikana katika maeneo yote muhimu ya urari wa mahesabu ya mwaka.''Benki yetu inajivunia kwa mara nyingine kupata faida kubwa ikilinganishwa na benki zingine shindani ikiwa na ongezeko la asilimia 44 katika biashara ya fedha za kigeni na ongezeko la asilimia 30 katika mikopo.Pichani shoto ni Mkuu wa kitengo cha Fedha na Utawawala Bwa.Joseph Mabusi pamoja na mwisho kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Bwa.Sylvester Bahati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...