Na Ndugu Kagutta N.Maulidi |
Tunapoendelea kufuatilia majadiliano ya wajumbe maaluum wa bunge la katiba si vibaya tukaweka msisitizo au kuwakumbusha wajumbe wetu kuhusu mada iliyopo katika rasimu ya katiba sura ya tano inayozungumzia urai pacha.
Nchi yetu bado haitambui uraia wa nchi mbili, kwa maana kuwa ukichukua uraia wa nchi nyingine unapoteza haki ya Urai wako wa Tanzania.
Tunashukuru kuwa swala hili limeingizwa katika rasimu ya pili ya katiba,ili liweze kujadiliwa .Sisi Watanzania tunaoishi nje ya nchi ni matumaini yetu kuwa wajumbe wa bunge maalumu wataliangalia swala hili kwa mapana zaidi na kulikubali kwa faida ya watanzania na nchi yetu kwa jumla.
Wengi wa watanzania wanaoishi nje(Diaspora) wamelazimika kuomba uraia wa nchi wanazoishi ili kupata haki zao baada ya kuishi na kufanya kazi kati katika nchi hizo kwa muda mrefu.
Nikweli kwani jambo hili lina faida nyingi Zaidi kuliko hasara.
ReplyDeletena ukiangalia karibu nchi zote Duniani zina raiya pacha.
Jirani zetu Kenya na Uganda wapo na Raiya pacha.
HIVI HAWA JAMAA WATANYAMAZA LINI NA HILI SUALA LAO???DAH ISHAKUA TAABU SASA KILA PAGE UFUNGUAYO??? WENGINE HATA NAULI ZA KURUDI KUJA KUZIKA AU KUSALIMIA NDUGU ZAO WA KARIBU HAWANA BADO WANATAKA RAIA PACHA......
ReplyDeleteAnonymous hapo juu unae shangaa kuwa kwanini Diaspora wanendelea kudai uraia pacha.Nihivi kama issue hii huifahamu sawa x2,tafuta mtu akujuze au nyamaza waache wanaofahamu wachangie.
ReplyDeleteIt is truee, it is just too much. But the question of going home is a personal matter. I haven't been there for 20 years and I don't miss a thing still I communicate with all my relatives etc by email, telephone etc and also I do send monies now and then. They have never complained. Mazishi ni swala la wabongo, I don't need to be there kuonyesha nimefiwa, nawasaidia kwa pesa na wote hawalalamiki.
ReplyDeleteHili swala muda muafaka bado . Kwa nchi zetu za kiafrika. Hapa swala la uzalendo hamna. Hawa wanaotaka uraia pacha walikimbia mzazi wao (Tanzania) kwenda wakati nchi ikiwa na hali mbaya.. Na kwenda ughaibuni kwenye malisho ya kijani...Sasa fursa zimefunguka ? Wanataka huku na kule...?? Mguu ndani mguu nje..mambo yakiharibika mtukimbie. Kama ni hizo remittence mtutumie tu ndugu zenu..na kama mna mtaji wa kutosha karibuni muwekeze. Kawa wachina ,wa S.afrika na wengineyo wanavyowekeza..kama mnauzalendo wa kweli karibuni Tanzania tutawapokea kama wana mpotevu aliaamua kurudi kwa wazazi wake..mkane uraia wenu huko. Mrudi tujenge Tanzania pamoja.. Sio mmesikia gesi urani na mafuta ndo mnakumbuka UTANZANIA?.. URAIA PACHA HAPANA.
ReplyDeleteTanzania tuna mambo mengi ya kuyafanya ili maisha ya wanannchi yawe mazuri ambao ndio wengi zaidi ya asilimia 80,watoto hawana madawati shuleni.matibabu bado wengi hawayapati,rushwa nk Kwa nini serikali ipoteze muda wake kwa watu ambao wengi wao waliondoka nchini kujilipua na ili wapate ukimbizi ilibidi watoe malalmiko kuwa Tanzania wanaonewa na maisha yao yapo hatarini?Kama ni kuwekeza Wachina hawana uraia wa Tanzania laki i wanawekeza,mtu anaeishi kwa welfare ina maana hata chakula kinamshinda inabidi serikali imsaidie nyumba,matibabu nk atawekeza nini?Tuwe na uzalendo kama Mugabe uwe raia wa Zimbabwe au Uingereza!
ReplyDeleteKuna maoni ya mtu asiyesoma hapa hajui anachosema na hajui anaochofikiria, anasema tu kwakuwa ana mdomo ndio maana kaandika maoni mengi yeye mwenyewe. Unajuha nchi ya Tanzania sio ya mtu ni ya watanzania wote mtanzania aliyezaliwa mtanzania ataendelea kuwa mtanzania kwa maisha yake yote hata kama ana urahi wa nchi kumi. wewe ukileta wivu utakufa na kinyongo URAHI PACHA UTAKUJA KWA NJIA YEYEYOTE HILE.
ReplyDeleteUnasema ulikuwa nje miaka 20,nafikiri ulikuwa kinyume cha sheria huko ulikokuwa, sasa huna asila na wengine ambao WANAISHI KISHERIA,Hawa hawajakunyima wewe visa za kukaa huko kihalari. Acha wivu na utafanikiwa kimaisha unarudi nyuma kwasababu ya wivu na kinyogo. jifikirie. URAHIA PACHA OYE
Hivi wadau wa diaspora, nyinyi hoja yenu ni uraia pacha tu juu ya taifa letu? Rasimu inamengi mno lakini michango ya diaspora ni uraia pacha tu. Hapa UK wanaopenda utanzania wao wamebaki nao na kugonga muhuri wa ukaazi wa kudumu na wanapata haki sawa tu kama raia mwengine. Wenye kudai uraia pacha wengi wao hivi sasa sio watanzania walijifanya waburundi, somali, congo etc. Tulieni msipeleke mashaka nyumbani.
ReplyDeleteSwala hili naona limegubikwa na chuki na wivu zaidi kuliko uelewa.
ReplyDelete-Pamoja na kwamba nchi yetu haiwezi kufuata kila linalofanywa na wenzetulakini si vibaya kujiuliza kuwa majirani zetu wote ambao kimsingi wanachangamoto zinazo fanana na zetu wameruhusu uraia pacha.Na mpaka sasa hatujasikia madhara ya uamuzi huo zaidi ya kusikia faida zake.Mfano katika hotuba alioitoa Raisi Kenyetta wakati akiwa Marekani hv karibuni alishukuru mchango wa diaspora katika kujenga uchumi wao kwa kuingiza zaidi ya Ksh.40bilion ktk mzunguko.Je, sisi hatuoni kuwa hilo litakuwa na manufaa?
-Kuna mchangiaji ameuliza kwanini diaspora hawachangii hoja nyingine za kikatiba isipokuwa la uraia pacha.Nadhani kwa binaadamu yoyote wa kawaida si rahisi kujihusisha na swala lolote mpaka wewe mwenyewe uhusishwe rasmi.Hii ikiwa na maana ya kuwa mchango wao utakuja mara baada ya kupishwa kwa uraia pacha.
-Swala la kusema hawa watu walikimbia nchi yao, na sasa wanataka kuwa huku na kule halina maana.Hivi msukuwa, mhaya,mchaga alie hamia Dar es Salaam au mkoa wowote kwa msingi wa kutafuta maisha anapaswa kukanwa na jamii yake kwa kukosa uzalendo.mipaka ya hizi nchi katika karne hii imebaki ya kisiasa zaidi kuliko ya kiuchumi.Diaspora wako katika kutafuta kama ambavyo mtu yoyote yule alie nje ya makazi yake ya asili, kinacho wabana ni sheria tu.
Ni vizuri mnatafuta maisha ughaibuni...na sidhani kuna swala la wivu hapa. Wivu kwa kipi?? Ulaya na amelika? Nadhani bado mna fikra na mitazamo wa watanzani wa enzi za mwalimu...sikuhizi kuna hata ndugu au rafiki anayekuagiza "raba mtoni" ,nguo au hata simu .??? Mnarudi tunawaona mnakaa mwezi miezi miwili mbio zinawashinda..tanzania ya sasa sio mlio iacha..Mjipange mlete new idea kutoka huko tujenge nchi ...na yote hii mnataka ARDHI tu..bado ni watanzania nasisitiza Tena Rudini Tujenge Nchi yetu Pamoja..
ReplyDelete