Bw. Shirwan Naseh, raia wa Netherlands  mwenye asili ya Iraq aliyezuiliwa kuingia nchini na kupigwa pigwa PI na Idara ya Uhamiaji



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hongereni kwa kazi nzuri. Na wale Raia wa Uturuki pale Kawe wanaouza Malumalumu na vitu mbalimbali vya ujenzi ningeshauri wachunguzwe Kwani kila bidhaa utayouliza hawana zaidi ya iliyoko ktk display. Na ukiangalia godown ni kubwa na hadi wafanyakazi wao hawawaelewi nini hasa kimewaleta. Nilitaka bidhaa pale nikaambiwa hadi miezi miwili ndio mzigo utakuwa umekamilika nikaenda baada ya miezi miwili ni kaambiwa miezi miwili tena. Sasa nikajiuliza kundi lote lile la Waturuki wamekuja kufanya nini hapa nchini? Natoa angalizo Raia wote wa kigeni nchini hawawezi kuwa na nia njema na nchi yetu. Kwani kuna makundi ya raia wa Sauz Africa na zambia wanaishi na kufanya kazi kwa visa za utalii.Na nimesikitika kuona wengine wanavyovitambulisho vya uraia wa Tanzania ambavyo wengine hata hatujavipata. Msinichukie maana majirani zetu tuliowabeba ndio wanatutukana leo na kutuona mapunguani.

    ReplyDelete
  2. Nadhani kuna jambo kubwa ambalo sisi hatujalifahamu ambalo linafanya wageni haramu na halali waing'an'ganie nchi yetu.je, udhaifu wa ufuatiliaji ,corruption au ni urahisi wa kuondosha rasilimali.

    ReplyDelete
  3. The mdudu,Tanzania inakoelekea ni hatali sn hao uhamiaji wanatakiwa waamke usingizini wachape kazi usiku na mchana na MISAKO KWA WAGENI WANAOISHI KIMAZABE,,lakini kwa mwendo huo wa moto wa kifuu tutakuja kujuta muda si mlefu,,na ningependa mlishilikishe jeshi letu tukufu la JWTZ katika hiyo misako ya wageni au wahamiaji haramu coz naliaminia jeshi langu ili tuisafishe nchi yetu,,mje na kitu SAFISHA NCHI YETU ILUDI KAMA ZAMANI.

    ReplyDelete
  4. Kwanza naungana na msemaji wa hapo juu kwa maoni yako, ktk habari iliyopita kuhusu wale raia wa Iraq waliokua na pass za Sweden....niliuliza hapa ktk kutoa maoni yangu kwamba 'kwanini Tanzania??je yawezekana kuna waliofanikiwa kabla yao???sasa ktk habari hii ndio napata majibu yangu! Kiukweli insikitisha sana nchi kufanywa kama nyumba isiyo na mlango...huu ni mwaka wangu wa kumi naishi Ulaya tena ktk nchi tofauti..hakika hawa wenyeji jinsi walivyo makini ktk maslahi ya mataifa yao yaani sijapata mfano....mgeni utaendelea kua mgeni hata kama utaishi milele na hutokua na nafasi ya kujipenyeza zaidi hata uwe nani...yaani kuna kiwango ambacho utaweza kufika kwa kujipenyeza ila sio chenye kugusa maslahi ya Taifa...jukumu hili ni la wote si lakini huko kwetu hali ni Tofauti....Cha wote ni hatari sana kwa vizazi vijavyo yaani ...sijui hili kama linatazamwa....

    ReplyDelete
  5. Sasa hawa wachina wanaouza mitumba kariakoo mbona mnawanyamazia tu na kuwatupia kisogo?

    ReplyDelete
  6. Hongeren Uhamiaji, Hayo Ndiyo madhara ya vita, Na hatujajua hao watu wanaokimbilia huku wana mchango gani katika hizo vita zinazoendelea katika mataifa Yao, Usikute wamewasha moto na Sasa wanakimbia.Hapa kuna la kujifunza..

    ReplyDelete
  7. Jana niliandika waraka mrefu wizarani kuhusu ajira za Watanzania ziko hatarini na hakuna hata kiongozi mmoja anapigia kelele, wageni ni wengi na wanapewa kipaumbele sana kwa kazi ambazo Watanzania wanaweza. Kampuni binafsi usiseme wamejaa tele, Hui ni uzembe mkubwa wa wizara husika. Jamani wananchi tunatakiwa tuamke kupigania ajira zetu name utanzania wetu.

    ReplyDelete
  8. Tunakimbilia ulaya, wa ulaya wanakimbilia kwetu!!!!

    ReplyDelete
  9. Tatizo kubwa ni RUSHWA!! Hao wanaotoa vibali vya kazi, nikweli kama hawajui ni ajira gani ama biashara gani zifanywe na wazawa ama wageni!! Huo ni Uozo wakutupwa. Tunauza Nchi yetu kwa bei chini, Viongozi wameishi nje wanajua.

    ReplyDelete
  10. Hongereni watu wa uhamiaji. Hata hivyo kuna baadhi yenu wanendekeza rushwa na udini. Kuna baadhi ya watanzania wanapoona mtu Fulani katoka kwenye nchi ya dini anayoamini yeye basi huchukulia kuwa wale raia ni ndugu zake na hivyo hana budi kuwasaidia. Ubaya wa wageni unajulikana hata kama ni wa dini zenu.

    ReplyDelete
  11. Naamini sitokuwa nimefanya kosa kama nikisema kuwa uhamiaji ni wazembe mno. Hivi zile computer za finger prints katika viwanja vyetu ni za kazi gani?

    Taarifa inasema kuwa huyu jamaa amekuwa akiingia mara nyingi nchini, la ajabu ni kuwa passport yake tunaambiwa imetolewa July 2014, ina maana mara zote amekuwa anaingia na passport tafauti lakini computer pamoja na wafanya kazi wa uhamiaji wameshindwa kugundua kuwa mtu mmoja mwenye ameingia zaidi ya mara moja na passport tafauti, ilikuwa inatakikana mara ya kwanza tu alipoingia na passport tafauti computer zitowe taarifa na azuiliwe kuingia nchini.

    Naamini computer zilifanya kazi zake ila wana uhamiaji ndio walioshindwa kuwajibika aidha kiuzembe au kwa kulishiwa.

    MOJA YA MALENGO YA SYSTEM ZILIZOPO KATIKA VIWANJA VYETU VYA NDEGE NI KUZUIA MAJASUSI KUINGIA AU KUTOKA KATIKA NCHI YETU, NA NJIA PEKEE NI KUWA NA DATABASE YA FINGER PRINTS ZA KILA ANAEINGIA NA KUTOKA. NA KILA WAKATI MSAFIRI ANAPOCHUKULIWA FINGER PRINTS ZAKE SYSTEM INAANGALIA KAMA AMEFANYA FOJI YEYOTE TOKA JINA HADI AINA YA PASSPORT ANAYOITUMIA.

    ReplyDelete
  12. Hongereni sana uhamiaji na mlochangia hapo juu.. Nami naomba kutoa mchango wangu kwa jinsi nilivyojionea wenzetu Wa nchi za Ulaya wanavyolinda maslahi yao..Kwanza Idara itambue kuwa MTU kufanya kazi au biashara ..No lazima viza yako iruhusu kama ni tourist huwezi kabisaa kukubaliwa na ukikamatwaa no P.I unarudishwaa kwenu...na kibayaa zaidi hata wenzetu wa rangi zetu ..kwa chuki zao hudiriki kuwaripoti wenzao wanaoishi bila vibali... Ajira kwa wenzetu hutolewa kipaumbelee kwa raia wao kwanza ..na wageni huwa wa mwishoo kabisaa ....Hivyo basi changamoto isiwee ni hapo airport tu..ni vyemaa uhamiaji ianze Operation kwenye makampuni yote kubaini RAIA wanaoishi kinyemelaa na wawee serious kuwarudisha kama waaftica wanavyorudishwa huku bila hurumaa ! Na zaidi ajira ipewee kipaumbele kwa wazawa kwanzaaaa !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...