Waheshimiwa Wabunge walioitwa kusikiliza ajenda ya mtoto na kuhakikisha inaingia katika mchakato wa katiba.

kamati kuu la Baraza la watoto limekutana mjini Dodoma chini ya Uongozi wa mwenyekiti wake Ummy Jamaal kutoa tamko la watoto kwa waheshimiwa wabunge na waandishi wa habari wakitoa msisitizo wa ajenda ya mtoto kuwa sehemu ya mchaakato wa katiba.

Jambo kubwa walilosisitiza ni kuwaomba Ukawa warudi bungeni ili kumalizia mchakato wa kutengeneza katiba.
Mheshimiwa Sophia Simba, waziri wa maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati kuu ya baraza la watoto waliokaa pamoja Dodoma na kutoa Tamko lao mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya waheshimiwa wabunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...