Kampuni ya Bima ya Resolution mwishoni mwa wiki iliyoisha iliaanda hafla ya kufuturisha wateja wake katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hafla ilihudhuriwa na Sheikh Msaidizi wa Dar es Salaam, Sheikh Athuman Makumbaku.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Resolution Insurance nchini Tanzania, Bwana Oscar Osir alisema, "Tunawashukuru sana kwamba mmehudhuria hafla hii na tunawapongeza kwa uvumilivu wenu katika mwezi huu mkuu wa Ramadhan.”.

Naye Sheikh Makumbaku alisema, "Kwa niaba ya ndgug zangu Waislamu ningependa kuwashukuru Resolution Insurance kwa kutukumbuka wakati wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan. Pia ningependa kuwahimiza Waislamu wenzangu kutia maanani amri wakati wa Mwezi Mtukufu. Tuonesha upendo na uvumilivu kwa wote, kusameheana na kuwasaidia wale ambao hawana uwezo wa kujisaidia”.

Bwana Osir alimaliza kwa kusema, "Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu kwani ndiyo inatupa motisha ya kuendelea kuwapa huduma bora zaidi. Katika shughuli za kuwapa Huduma zilizo bora zaidi na zinazoweza kuwahudumia ukiwa hapa nchini na hata sehemu yeyote duniani. Ningependa pia kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwapa bidhaa bora na kuwasikiliza ili tutimize mahitaji yenu".
Meneja Mkuu wa Resolution Insurance, Oscar Osir akizungumza na wageni waalikwa wakati wa Futari iliyoandaliwa na Resolution Insurance iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Sheikh Mkuu msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Athuman Mkambaku akizungumza na wageni waalikwa wakati wa Futari iliyoandaliwa na Resolution Insurance iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wageni waalikwa wakipata Futari iliyoandakliwa Resolution Insurance iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya futari iliyoandaliwa na Resolution Insurance iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...