Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mchango uliotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kutoka kwa Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki .
Na Abdulaziz Kilwa Masoko
Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi wameendelea kunufaika na
wawekezaji,baada ya kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY
kuikabidhi halmashauri hiyo zahanati ya kijiji cha Nangurukuru ambayo
ujenzi wake umegharimu Tshs 262 Milioni .
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambayo yalifuatiwa na utiaji
sahihi mkataba wa ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo
ambazo ujenzi wake hadi kukamilika utagharimu shilingi 458 milioni Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki alisema
katika ujenzi wa zahanati hiyo kampuni ya PANAFRICA N imechangia jumla
ya shilingi 216,000,000.
Ambapo pia kutokana na tatizo la wafanyakazi
pia kampuni imeamua kufadhili ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa
zahanati hiyo ambazo mkataba wenye thamani ya shilingi 458,000,000
ulisainiwa baina ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw David
Roberts na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika hafla
hiyo fupi ya kukabidhi zahanati.
Aidha Kashangaki alibainisha kuwa sera ya kampuni hiyo licha ya
kufanya kazi ya uzalishaji wa Gesi ya songosongo pia hutoa misaada
kwa jamiii ikiwemo kufadhili programu ya ufundishaji lugha ya
kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari za
halmashauri hiyo,ambapo jumla ya shule za sekondari 20 kati ya 28
zimenufaika na programu hiyo.
'Wana kilwa tulianza kusaidia elimu ya kiingereza kwa kuzifikia shule
20 ila kwa umuhimu wa elimu kuanzia mwakani tutazifikia shule zote 28
za sekondari ikiwemo kusaidia upatikanaji wa Umeme Jua kwa shule
ambazo hazina umeme 'Alimalizia Kashangaki.
Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega licha ya kuishukuru kampuni
hiyo aliwataka wananchi kupuuza kauli zinazosemwa ikiwemo baadhi ya
Vyombo vya habari kupotosha na kudai Manufaa ya Gesi yapo katika
kijiji cha Songosongo pekee Na kubainisha baadhi ya maeneo
yanayonufaika ikiwemo hapo Nangurukuru,Njinjo ,Somanga na kilwa masoko
'Wananchi wa Kilwa nadhani ni mashahidi kampuni hii imesaidia wilaya
yote si Kama Gazeti moja lilivyoandika hivi karibuni Huu ni upotoshaji
mkubwa kwani elimu inasaidiwa wilaya yote,Afya Hivyo hivyo,Maji
wananufaika mpaka Njinjo na hata mrahaba unaolipwa na kampuni hiyo
zaidi ya Nusu inachangia katika sekta ya elimu Tuwe makini kuyajua
haya yenye ukweli si maneno tu ya vijiweni...Alimalizia Ulega.
Awali akifungua hafla hiyo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha
Nangukuru,Hamis Ligweje alisema kabla ya PANAFRICAN kufadhili ujenzi
huo,wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wahisani wengine
ikiwamo shirika la Action Aid walichangia walichangia jumla ya
shilingi Milion 46 ujenzi ambao ulikuwa wa kusuasua mpaka wahisani
hao walipojitokeza kusaidia kuikamilisha.
'Hakika tulishindwa kabisa na Tulifikia hatua ya Kumuomba Rais Kikwete
Kusaidia alipokuja katika ziara yake ambapo aliwaagiza Viongozi wa
Wilaya kuangalia uwezekano ndipo Mkurugenzi aliehama Bw Mapunda
Alifanikisha kuwaomba hawa wahisani na leo wametukamilishia na
tunafarijika zaidi walipoamua kutujengea na Nyumba 2 kwa 4 za
watumishi itasaidia sana si kwa Nangurukuru tu hata wasafiri
watakaopata dharula katika barabara kuu.
Licha ya kukabidhi Zahanati hiyo Mkurugenzi mkuu wa Pan African
Energy,David Roberts Alikabidhi Vitanda Viwili vya kujifungulia akina
mama ikiwa ni hatua ya awali ya kuokoa Akina mama katika suala la
Uzazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...