Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda (Katikati) akiongea na Wanahabari (Hawapo pichani) kuhusu makocha wa Timu ya Barcelona kutoka nchini Hispania ambao wako nchini kwa ajili ya mafunzo ya makocha wa Tanzania yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili.Wengine picha toka kulia ni Balozi wa Spain nchini Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,Kushila Thomas,Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes,Kocha Daniel Bigas Alsina.mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Balozi wa Hispania nchini Tanzania Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis (Kulia) akiongea na
Makocha kutoka Timu ya Barcelona ya nchini Hispania katika mkutano wa Wanahabari uliofanyika
jijini Dar es Salaam jana (leo), makocha hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo ya siku mbili kwa
makocha wazalendo, wa kwanza kushoto ni Kocha Daniel Bigas Alsina na katikati ni Kocha Isaac Oriol
Guerrero Hernandes
Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes kutoka timu ya Barcelona ya nchini Hispania
(katikati) akitoa maelezo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya siku mbili watakayotoa
kwa makocha 30 wakizalendo.kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bi. Juliana
Yassoda na wa kwanza kushoto ni kocha Kocha Daniel Bigas Alsina.
Makocha wa Kizalendo 30 ambao wanatarajiwa kupewa mafunzo ya siku mbili kutoka kwa
makocha wa Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja
Picha zote na Benjamin Sawe kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM
Hivi sasa Barcelona na Spain mpira wao umeshajulika hivyo timu zitakazo fuata mfumo wa Barcelona, Brazil na Spain hazitafika mbali. Mfumo mzuri wa kuigwa sasa ni mfumo wa Real Madrid, Atletico Madrid, Ujerumani na Argentina.
ReplyDelete