MKE
wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dorcas Membe
amekitaka kituo cha kusambaza Matrekta kwa wakulima cha Kariati Matrekta
kupunguza tena bei za bidhaa hizo ili kuwa kimbilio kwa wakulima.
Kauli
hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaa wakati akizindua kituo hicho
ambapo alisema ingawa bei zao zipo chini wapunguze tena ili hata mkulima
wa chini aweze kumudu kununua au kukopa trekta hiyo imuwezeshe
kuondokana na umasikini.
Akizungumza
katika uzinduzi huo alisema anapongeza uanzishwaji wa kituo hicho kwani
ni kazi inayowahusu wakulima ambao idadi yake ni takribani asilimia 80.
''Nakupongeza
Mkurugenzi kwa jitihada za kuanzisha kituo hiki chenye lengo la
kuwawezesha wakulima kupata matrekta na zana zake kwa fedha tasilimu au
mkopo, mpango huo utawakomboa wakulima wengi kuondokana na jembe la
mkono'' alisema
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kariati Matrekta, Alhaji Omary Kariati alisema jambo ambalo
wanalifanya ni kuunga mkono mpango wa Kilimo Kwanza wa serikali ya
awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete kwa vitendo.
Aidha
alisema kwa kuhakikisha wakulima wanapata dhana za kilimo hadi sasa
tayari wamesambaza matrekta 80 ambapo wamekuwa wakikopesha bila ya
dhamana.
''Nimeisikia
mama akisema kuwa tupunguze bei na namuhakikishia hapa hapa kwamba
tumepunguza tena bei trekta la milioni 23 litanunuliwa kwa shilingi
milioni 20''alisema
Mbali na hayo Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo amesema wanashirikiana vema na kituo hicho hivyo wakulima wategemee mambo mengi mazuri.
Mke
wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas
Membe (katikati), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha
Kusambaza Matrekta cha Kariati Matractor kilichopo Kinondoni Dar es
Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Omary Kariati na Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB,
Victor Malewo, ambapo wamekiwezesha kituo hicho kupata mikopo ya
kununulia matrekta hayo.

Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati
Matractor , Omary Kariati wakionesha tovuti ya kituo hicho baada ya
kufungulia. Tovuti hiyo ya www.kariatimatractor.com itamsaidia mkulima
yeyote aliopo nchini kupata fomu kwa ajili ya kununua matrekta hayo.
Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe akisoma taarifa yake kwa wanahabari.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati
Matractor , Omary Kariati (kulia), akizungumza na wanahabri na wageni
waalikwa kwenye ufunguzi huo wa ofisi yake.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...