MACHINE HII NA VIFAA VYAKE ILIIBIWA NCHINI TANZANIA NA KUUZWA NCHINI ZAMBIA MJINI LUSAKA. BAADA YA JITIHADA YA POLISI WA TANZANIA, POLISI WA KIMATAIFA NA POLISI WA ZAMBIA MACHINE ILIPATIKANA MWAKA 2013 LUSAKA IKIWA INATUMIKA NA WATU WALIYOINUNUA.
MHE BALOZI GRACE MUJUMA AKIMKABIDHI MACHINE DR. NICOLAUS MBILINYI MGANGA MKUU WA WILAYA (DMO) YA MOMBA ILIYOKUWA IMEIBIWA MWAKA 2012. KUTOKA KUSHOTO NI DEREVA ALIYEKUJA KUCHUKUWA MACHINE, DR LAWRENCE MWAMPASHI (DISTRICT AIDS CONTROL COORDINATOR) MHE. BALOZI GRACE MUJUMA, DR. NICOLAUS MBILINYI NA MTAALAM WA MACHINE HIYO AMBAYE ALITHIBITISHA KUWA MACHINE NDIYO YENYEWE AKIWA NA AFISA UBALOZI Bw. RICHARD LUPEMBE AMBAYE HAYUPO PICHANI
Sasa, kweli kabisa mtu anaiba mashine ya kuhesabu CD4 akaifanyie nini au ndio anaipeleka kwenye hosptili yake binafsi. Kha! Iba nyingine tuwege na aibu jamani!
ReplyDeleteunafikiri mwizi ana akili msomaji mwenzangu. akija nyumbani kwako akakosa alichopanga kukuibia au kitu chochote cha thamani atakuibia hata kijiko. na usilogwe ukaacha kiporo chako cha wali na kisamvu chote atafagia kalaghabao. sijui huwa wanakuwa wamevuta bangi zinawapeleka msobe msobe na kuwasukuma kufanya vitu vya ajabu
ReplyDeleteMambo gani haya ya kuiba mashine za hospitali..
ReplyDelete