photo
Bw. Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013 Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.

Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni Tanzania pekee tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya kilimo Tanzania.
Dorice Mollel amesema “ hichi ni kitu cha muhimu sana nikiwa kama mrembo nikirudi nyumbani na kuieleza jamii inayonizunguka ili kutuletee faida baadae nchini kwetu”.
photo (1)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...