Mshambuliaji wa timu ya Kombaini ya Tanga, Kassim Jumaa (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Survey veterani, Ahmad Rasuli (katikati), wakati wa mchezo maalum wa kusherehekea Sikukuu ya Wakulima Nanenane uliofanyika kwenye viwanja vya Disuza mjini Tanga. Mchezo huo ulidhaminiwa na NSSF. Kulia ni Amir Athuman wa Kombaini ya Tanga.

Na Elizabeth Kilindi, Tanga
Timu ya Survey Veterani ya jijini Dar es salamu imeifunga timu ya Kombaini vijana  Veterani ya Jiji la Tanga 2-1 katika mchezo wa kuazimisha sherehe za wakulima nane nane viwanja vya Disuza vilivyopo Mkoani Tanga.
Mchezo huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ulikuwa na lengo la kukutanisha timu za maveterani ili kujenga mshikamano na kuhamasisha michezo.
Katika mchezo huo wachezaji wa savey Carlos Mdinga alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na wapinzani hatua ambayo ilisababisha gori hilo Dakika ya pili.
Aidha katika mchezo huo timu ya Savey ilionyesha makali yake ambapo dakika ya 40 walisawazisha goli kutoka kwa kiungo wake  Silyvester Malango.
Hata hivyo bahati nyota ilizidi kungaa kwa timu ya veterani baada ya Dakika ya 70 kupata goli la pili lililotiwa nyavuni namshambuliaji wake David  Emanuel.
Katika mchezo mwengine ni kati ya Timu ya Best point veterani imeibuka na ushindi wa goli mbili dhidi ya  Kombaini ya wazee Veterani ya Jijini Tanga.
Magoli  ya Best point yalifungwa na Sadiki Salumu dakika ya saba na goli la  pili lilifungwa na Miraji Paulo dakika za lala salama.
Baada yakumalizika kwa mchezo huo kocha Seleman Mgaya ambaye ni Katibu wa Survey Veterani ya Dar es salaam amesema wamefurahishwa ushirikiano unaotolewa namfuko wa hifadhi ya jamii NSSF hasa kwa kuonyesha mchango wao katika michezo.
“Tunaishukuru sana  NSSF kwa moyo wa kutukutanisha pamoja kimichezo hatua ambayo tunajivunia kwaniwao wametambua umuhimu wetu hivyo hatuna budi kutoa ushirikiano”amesema Mgaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...