Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete walitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na mawasiliano.
Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo katika Tanzania.
Rais Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani ya Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea sehemu ya mfano wa ofisi ya kupangia mikakati ya Ikulu ya Marekani iliyotumika na Rais MStaafu George W. Bush kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library).
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoka kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library).
Jengo zuri, Tunahitaji institute kama hii kwa ajili ya kizazi hiki na kichacho kutukumbusha mchango wa Mwalimu nyerere katika kujenga taifa la Tanzania, kutathmini sera mbali mbali za nchi nk.
ReplyDeleteHapo kuna mengi sana ya kujifunza.
ReplyDelete1. USA inatuonesha thamani ya vitu tulivyonavyo lakini tunavichezea
2. Mkuu ameguswa na anawaza kitu moyoni
3. Watanzania tunakila kitu cha kutufanya tuwe na maisha mazuri. Tatizo ni ujanja ujanja usio na maana hasa kwa viongozi wetu.
4. Hatuna uchungu na Taifa, tunawaza matumbo na familia zetu tuu.
5. Angalieni kero ya ardhi inavolitafuna Taifa. Wahindi wanamilikishwa ardhi kuuubwa miaka 99 wanalipa Tshs 600 kwa ekari moja. Hii bei walipewa tangu tupate uhuru hadi leo. Je viongozi hawana mkakati wowote wa kulinda ardhi na kuingiza fedha kupitia ardhi.
6. Viongozi wapo busy kwenda ulaya na kudaka misaada wakidhani ulaya ndio solutuion ya matatizo yetu.
7. Solution ya matatizo yetu ipo kwichani mwetu na si Ulaya.
Mia
Wewe Mbona una masihara, cc ni wakutizama tuu watu wanafanyaje, lkn kwetu ni mkono kwenda kinywani basi
ReplyDeleteMdau wa kwanza, makumbusho ya Mwalimu ipo kijijini Butiama. Unaweza kuangalia https://www.youtube.com/watch?v=xSoAZBRTTWQ
ReplyDeleteHii inatupa wazo ya kwamba JK nae pia anaweza kujenga kwao Msoga au anagalu Bagamoyo. Tunweza kuanza machango hata kabla haja staafu. Hii itatuwezesha na si tuone medali [nishani], vyeti vya shahada ya heshima [honoris causa] na zawadi nyingine JK aliyoipokea kwa kupitia nafasi yake ya Urais.