o3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.o6 o7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014o8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014
o2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.

 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Nampongeza rais kwa juhudi za kukuza investment in Tanzania na kutumia kila opportunity inayojitokeza. Lakini nasikitika sana na jinsi ambavyo ofisi za serikali anayoiongoza zilivyo inefficient.

    Ni vipi watanzania wataweza kushindana katika ajira kama wale wanaotuongoza they can't manage their office maana wanaintroduce unnecessary complexities ambazo zinakuwa bottleneck kwa watanzania wengi?

    Leo nimeenda kwenye ofisi ya serikali, hii ni wiki ya pili sasa, na nimepigwa wiki ya tatu mpaka next week. Kuna certificate natakiwa kupewa kwa ajili ya shughuli zangu ambazo ni kijiendeleza kielimu. Nilichoambiwa ni kuwa muhusika anayetakiwa kusign hicho cheti yuko kwenye msafara wa rais ulioenda Marekani.

    How can an office be closed simply because muhusika is not in the office? Kwani serikalini hakuna kukaimu office in order to maintain continuity, and promote efficiency?

    Why should the president include inefficient individuals kwenye msafara wake. If a person can not manage his/her office, how can this person manage the US-Africa investment?

    Watanzania tunafanya mzahaaa...we don't know what we really want.

    Muheshimiwa rais kuwa makini na hao ulioongozana nao wanakuangusha...huku Tanzania wamefunga office, yaani mambo yamesimama eti mpaka warudi wao!!!!



    ReplyDelete
  2. Nani anabisha?

    Moja kwa moja tusikakamaliane misuli ya shingo kwa mabishano Mhe. Raisi Jakaya Kikwete na yeye ni miongoi mwa Mabosi wa dunia hii ya Mwenyezi Mungu!


    Watanzania wengi hatuelewi ya kuwa tuna Rais bora Ulimwenguni!!!

    Wapo watu wa nchi nyingi sana duniani hasa hawa majirani zetu Kigali, Nairobi, Kampala na kwingineko walitamani wawe na Raisi kama JK lakini hawakujaaliwa kwa hilo!

    Pana Bosi wa Kampuni kubwa sana ya Mafuta wa nchi jirani ya Afrika Mashariki juzi niliona ktk Gazeti la Serikali la Daliy News akiomba Uraia wa Tanzani!,,,HUYU NI MMOJA KATI YA WAJANJA AMBAO WAMEONA UMUHIMU WA KUWA MTANZANIA NA WENGI TUTAWASHUHUDIA SIKU HADI SIKU!.

    Kwa nini yeye Mhe. Raisi JK ni mmoja wa MaBosi wa Dunia?

    1.Tanzania imekuwa na kasi kubwa ya maendeleo duniani kwa 7% ya pato la taifa GDP.

    (Wale wabishi msilete malumbano ya kulinganisha ukuaji huu na hali halisi za watu kwa kuwa ugawaji wa ukuaji (economic inclusion) hilo ni tatizo na changamoto za nchi nyingi duniani labda wewe na mimi tutafute jawabu lake na sio kulaumu ya ''KUWA UCHUMI UMEKUWA KATIKA MAKARATASI NA TAKWIMU NA HALI HALISI HAIFANANI NA SIFA ZINAZOTOKA'')

    2.Mhe. Raisi JK amepokea Tuzo ya Utawala bora na ukuzaji wa uchumi na maendeleo kwa Afrika.

    3.Kwa mara ingine tena Mhe. JK anapata Tuzo ya Demokrasia na Ustawi kwa Afrika.

    NANI ANABISHA YAKUWA MHE. JK SIO BOSI WA DUNIA?

    VIVYO HIVYO WALE WANAOGOMBEA KUUTAKA URAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 2015 WANATAKIWA WAWE NA VIWANGO.

    TANZANIA SIO NCHI YA KUTAWALIWA NA WATU WENYE SIFA ZA CHINI NA VIWANGO VYA UONGOZI, HILI NI TAIFA MUHIMU LA DUNIA KWA SASA.

    WANAO UTAKA URAISI 2015 WANATAKIWA KUWA NA SIFA KAMA ZA JK WASIO KUWA NAZO ILE HATA KUTAFUTA KUPENDEKEZWA WASIJISUMBUE KWA KUWA WATAAIBIKA BURE WATAUKOSA URAISI!!!

    ReplyDelete
  3. Mwaka jana mwishoni nilipotoa Maksi 197% (MIA MOJA TISINI NA SABA KWA MIA MOJA SIO MAKOSA YA UCHAPAJI) kwa Mhe. Raisi Jakaya Kikwete wengi humu jamvini walinipigia makelele saaana!

    1.Magogoni Darisalama kwa Mhe. JK mwaka jana 2013 ilikuwa ni maskaniya wageni hasa Maraisi na Wakuu wa dunia nzima, dunia nzima iliwasili kwa JK kama tulivyo shuhudia na hazi sasa wakimiminika kuja!

    2.Haukupita muda mwanzoni mwa mwaka huu 2014 Mwezi wa Aprili Marekani ikatoa Tuzo ya Utawala Bora kwa Afrika kumpa Mhe. Raisi JK!

    3. Mwezi uliopita Julai- 2014 Tuzo nyingine ya Demokrasia na Maendeleo inatolewa kwa Raisi JK kutokea Uholanzi!

    4.Tanzania mwezi Mei-2014 inatangazwa na Benki ya Dunia kuwa na kasi kubwa ya maendeleo duniani.

    5.Katika Mkutano wa Viongozi wa Afrika Marekani Agosti-2104 Mhe. JK anakuwa meza kuu na Mtoa Hotuba!

    JE WATANZANIA WENZANGU MIMI NILIFANYA MAKOSA MWAKA JANA KUMPATIA MHE. RAISI JAKAYA KIKWETE MAKSI 197%?

    KWA MUENDELEZO WAKE HUU KIUTENDAJI ULIOTUKUKA DUNIANI MNAONAJE NIKIMPA MAKSI NYINGINE ZA ZIADA 200% zikafikia 397% nitakuwa tena nimekosea ?

    ReplyDelete
  4. Kenya ilikuwa inashida kama hizi za kukosa ufanisi serikalini na kupiga tarehe watu wanaohitaji huduma wakaanzisha Huduma Centres ili kuharakisha huduma kwa wananchi. Pengine na sisi tunahitaji kitu kama hiki. Kama shida ni kutumia mafaili kuimarisha masijala zetu kwa teknolojia za kisasa kutasaidia.Jamaa mmoja alitaka kwenda kulipia kiwanja sehemu fulani Pwani akaambiwa muhusika hayupo leo njoo kesho. Huu ni ukiritimba ambao tukinuia tunaweza kuuondoa.

    ReplyDelete
  5. Tuache upotoshwaji wa takwimu na sifa zisizo na tija! Umahiri wa kiongozi inapimwa na hali ya wananchi wala sio "Tuzo" zinazotolewa na taasisi ambazo hatujui zina nia gani!

    Na hicho kipimo cha "GDP" kimepitwa na wakati, tunatakiwa tujitambue na kuanza kutumia akili zetu kuchambua mambo, sio kutumia akili za kukopa kama alivyotwambia Mh. JK. La sivyo tutazidi kujichimbia kwenye shimo wakati wajanja wanaendelea kuifaidi nchi yetu!!

    ReplyDelete
  6. Watanzania msichanganuywe na hizo tuzo wala kura za maoni za huko nje, tuangalie Kiongozi wetu anatufanyia nini. Kwa mfano kura za viongozi katika Afrika wa kwetu yuko nafasi ya 10, chini ya hata wakongwe Paul Biya na Blaise Compaore! Sasa huwezi kujua hao wenzetu wanatumia vigezo gani, au wana nia gani!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...