Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada
ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya
kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la
Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda
(wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri
mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar
es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la
Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda
(wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya
waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar
es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia)
akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi
mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la
Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi
mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...