Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (katikati) akiingia katika kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii.  Wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) na  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (Kulia).  Kongamano hilo lilitayarishwa na TPSF pamoja na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (Kushoto) akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii.  Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu; Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa VICOBA na Mbunge Viti Maalum, Bi. 
========  ========  ==========
Taasisi za fedha nchini zimeshauriwa kulegeza masharti ya utoaji mikopo ili wajasiriamali nchini waweze kupata fursa zaidi ya kupata mitaji kuendeleza biashara zao na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam. Waziri huyo alisema Jumanne wiki hii kuwa taasisi za fedha nchini zilegeze masharti ili wajasiliamali waweze kupata mitaji ya biashara zao.
Kongamano hilo lilitayarishwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Financial Sector Deepening Trust (FSDT). “Ninayo furaha kubwa kuona TPSF na wadau wengine wameandaa kongamano hili ambalo linalenga kutafuta suluhisho la wajasiliamali kupata mitaji kutoka taasisi za fedha,”alisema.
Alisema moja ya changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo ni namna ya kupata mitaji kutoka katika taasisi hizo, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya biashara. Alisema mikopo kutoka benki inatolekewa kwa masharti makubwa na riba kubwa jambo ambalo ni kikwzo kwao na taifa pia.
“Sera ya nchi inaruhusu sekta binafsi kuendesha uchumi kupitia kampuni ndogo, za kati, na wajasilimali, sasa mitaji kwa wajasiriamali ni jambo ambalo haliepukiki,”alisema. Alisema serikali inashirikiana na TPSF kuhakikisha mazingira ya biashara yanaimarika na kongamano hilo ni moja ya hatua muhimu katika kuondoa vikwazo hivi.
Aidha alisema wakati nchi inasubiri kuingia katika uchumi mkubwa kutokana na gesi na mafuta ni lazima wajasiriamali wadogo wawezeshwe ili pia wawe na uwezo wa kutoa huduma kwa kampuni kubwa. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji TPSF, Bw. Godfrey Simbeye alisema kongamano hilo ni la muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa mitaji  kwa wajasiliamali ambao ni tegemeo kubwa katika kuendeleza nchi.
“Nchi zilizofanikiwa zimewekeza katika maendeleo ya wajasiriamali wao, hatuna budi kufanya hivyo,” alisema. Alifafanua kuwa wajasiriamali wakipatiwa huduma za fedha na kukuza mitaji yao, wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo.“Tumeshuhudia ukuaji wa mitaji na uchumi wetu unakwamishwa na mambo mengi mojawapo ni namna ya kupata mitaji,”alisema.
Alisema mitaji mingi inatoka benki lakini kwa  mazingira yaliyopo ni vigumu kwa biashara inayoanza kupata mitaji kutokana na masharti ambayo siyo rafiki. Alisema sekta hiyo lazima iwezeshwe sababu ndiyo yenye uwezo wa kutoa jira kubwa na kuleta mapinduzi ya uchumi.
Naye Mtaalamu wa Maswala ya Wajasilimali, kutoka FSDT, Bw. Peter Kingu alisema kuna kila sababu taasisi za fedha kupanua wigo kwa wajasilimali kupata mitaji bila ya kuweka masharti magumu. “Taasisi yetu inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo TPSF katika kuhakikisha wajasiriamali wanaimarika kibiashara,” alisema.
Kongamano hilo lilishirikisha wadau mbalimbali toka sekta binafsi, sekta ya umma, taasisi za utafiti, kampuni mbalimbali pamoja na benki miongoni mwa wadau wengine. Kampuni ya simu za mkononi ndiyo iliyodhamini kongamano hilo. Inatarajiwa kuwa maazimio ya kongamano hilo yatasaidia katika juhudi za kurahisisha upatikanaji wa huduma za fedha miongoni mwa wajasiriamali wadogo na wa kati hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...