Vijana wabarikiwa wakiwa katika ibada ya ubarikio kabla ya shughuli ya kuwabariki

Usharika wa Kikristo wa Kiswahili, ulio chini ya kanisa la kiinjili la kilutheri marekani, umebariki vijana tisa kwa mara ya kwanza kuwa washarika kamili. Tukio hili la kihistoria lilifanyika Jumapili iliyopita (8/24/2014). 
Mara baada ya ibada ya ubarikio, vijana, familia, ndugu, jamaa na washarika wote walielekea katika ukumbi wa mji wa Shoreview kwa ajili ya mapokezi ya vijana hao na chakula cha jioni. 
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Mchungaji Dk. Joseph Bocko, kutoka Chicago, Illinois, ambaye ni mkuu wa idara ya huduma za injili za kiafrika kwenye makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kiluteri la Marekani (ELCA); Mchungaji Deborah Stehlin, ambaye ni msaidizi wa askofu wa Sinodi ya maeneo ya Minneapolis katika mambo ya misheni ya injili; Mchungaji Phares Kakulima ambaye ni Askofu mdogo wa jimbo la Karagwe, na Douglas Mmari, ambaye ni mwanafunzi wa uchungaji; bila kumsahau Mchungaji Andrea Mwalilino ambaye ndiye mchungaji wa Usharika wa Kiswahili wa
Minnesota katika kanisa la Holy Trinity kusini mwa jiji la Minneapolis. Katika ibada hiyo maalum, pia kulikuwa na ubatizo wa watoto watano, na vijana wawili.
Baada ya kubarikiwa, vijana waliimba wimbo wa “Servants Prayer” kama sala yao ya shukrani ya ubarikio, wakisaidiwa na muimbaji mashuhuri wa kikristo, dada Rachel Kurtz. Kabla ya kubarikiwa, waliimba na dada Rachel wimbo wake wa Hallelujah.
Vijana wabarikiwa wakisubiri usafiri maalum kuelekea kwenye ukumbi wa mapokezi mjini Shoreview.
Vijana wabarikiwa wakisubiri usafiri maalum kuelekea kwenye ukumbi wa mapokezi mjini Shoreview.
Picha ya pamoja ya wabarikiwa pamoja na jopo la wachungaji lililowabariki (aliyekosekana katika picha ni mchungaji Deb Stehlin from MN Area Synod)
Vijana wabarikiwa wakipiga picha ya pamoja na Father Herbert Gappa, mmisionari aliyetumikia kanisa la katoliki huko Mwanza na Shinyanga kwa miaka karibu arobaini.
Vijana wabarikiwa wakiwa nje ya ukumbi wa jumuiya wa Shoreview, mara baada ya kushuka kutoka kwenye “limousine” lililoandaliwa rasmi kwa ajili yao: Kutoka kushoto kwenda kulia ni Nana Kwame Anokye-Agyei (Wazazi Charles Anokye-Agyei na Jennifer Lobulu), Augustino Wema Sprita (Wazazi Timothy Shima na Anna Mtoi Shima), Loveness Shanalingigwa na Glory Shanalingigwa (Wazazi Oswald na Penuel Shanalingigwa), Eliwaza Patricia Dyauli (Wazazi David na Tasiana Dyauli), Jayness Kinambora Msuya na Lisa Naojwa Msuya (Wazazi Gracious na Florence Msuya), Maame Abena Anokye-Agyei (Wazazi Charles Anokye-Agyei na Jennifer Lobulu), na Ena Ndemange Mwalilino (Wazazi Andrea na Sarah Mwalilino).
“Ma-kipa imara” wakipokelewa ukumbini kwa nderemo, vifijo na vigelegele, chini ya mwongoza sherehe, Mwalimu Gracious Msuya. Pichani pia ni Mchungaji Mwalilino wa usharika wa Kiswahili Minnesota, na Mzee Charles Semakula, mwenyekiti wa baraza la uongozi wa usharika wa Kiswahili Minnesota.
Vijana kabla ya kukata keki ya ubarikio. Picha kwa hisani ya Emma Nagai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. George Kato PhillipAugust 31, 2014

    Safi sana Mchungaji wangu Bocco pale Ndolage parish Kamachumu bukoba tunakukumbuka sana na mkeo Jeska watoto atugonza nk.j

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...