Na Profesa Mbele
Kitabu hiki ni
mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo, uliotungwa na
Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi, uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali;
naMwanakupona, uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na
M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa
na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999.
Hizi ni kati ya tenzi
maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi
zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa
"classics."
Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi,
kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu
ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anayesifika kuliko
wote tangu zamani katika jamii ya wa-Swahili.
Alikuwa pandikizi la
mtu, mwenye vipaji kadhaa: kuwashinda maadui, shabaha katika kutumia upinde na
mshale, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi. Juu ya yote, alikuwa muungwana
sana, mfano wa kuigwa. Lakini alifanyiwa visa na ndugu yake ambaye alikuwa
mfalme, hadi hatimaye akauawa na kijana mdogo, ambaye alikuwa mpwa wake. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Simulizi ni nzuri sana....ila nasikitika wanafunzi wetu nyumbani hasa wa sasa wamepoteza ari ya kujisomea vitabu kama hivi......
ReplyDelete