Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa
habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina
la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa
Samora Jijini Dar.
======= ======= =======
Bwa.Peter alisema kuwa siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promosheni inayolenga
kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina
la BWERERE yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.
''Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na
maofisini ambao wanatumia huduma ya malipo
ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga
simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe,
Vilevile Promosheni hii
inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA) kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na
Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo''.Alisema Bwa.Peter Ngota.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...