Mhe.
Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (
mwenye mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wa Kuunganisha
Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti nchini. Anayeshuhudia ni Prof. Tolly
Mbwete, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania na mwakilishi wa Benki
ya Dunia, Tanzania.
Mtandao
huo umeunganisha Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti 22 nchini ambapo
Vyuo Vikuu mbalimbali nchini vinaweza kuwasiliana, kutoa huduma ya elimu
mtandao, maktaba mtandao, utunzaji wa taarifa na nyaraka, kufundishia,
kuendesha mikutano kwa kutumia huduma ya audio na video, kuhifadhi,
kutunza na kulinda taarifa.
Mtandao
huo Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti umeunganishwa na Mkongo wa Taifa
wa Mawasiliano ambapo unaziwezesha Taasisi hizo 22 kuwasiliana kwa
haraka na kwa wakati. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
imesimamia na kuratibu jukumu hilo la Uunganishaji wa Taasisi za Elimu
ya Juu na Utafiti kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
Aidha,
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Kampuni ya Simu Tanzania,
Taasisi ya Serikali Mtandao na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa pamoja
zitashirikiana kufanikisha matumizi Endelevu ya mtandao huo kwenye
Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti nchini kwa manufaa ya Taifa letu na
kuongeza kasi ya matumizi ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano.
Uzinduzi huo umefanyika Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa sekta ya TEHAMA nchini.
Imetumwa na Prisca Ulomi,
Msemaji wa Wizara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...