Katika kuweka msisitizo juu ya tamko lao juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014, umoja wa Asasi Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimefanya matembezi huru kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Maandamano hayo yamewahusisha pia wanafunzi wa shule za sekondari za Jitegemee, Kinyamwezi, Ilala, Chanika na Maji ya Chai.
 Picha ya pamoja ya wanafunzi na viongozi wa asasi za kiraia walioshiriki matembezi hayo huru ili kuweka msisitizo juu ya tamko juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014
 Afisa Miradi wa Forum CC, Fazal Issa aliyeshika kipasa sauti akifafanua jambo kwa wanafunzi walioshiriki matembezi hayo.
 Matembezi huru yakiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...