Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Viongozi wa Kidini wanapaswa kuwa macho katika kuzikataa choko choko zozote na ushawishi unaotolewa na wanasiasa kwa kuzingatia maslahi yao badala ya manufaa ya Taifa zima.

Alisema kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na Viongozi hao wa Kidini ni kuwaombea watu wakiwemo Viongozi wa Nchi ili Baraka ziongezeke ndani ya Taifa pamojana umma jambo ambalo litasaidia kupunguza misuguano.

Balozi Seif alisema hayo wakati akilifungua Tamasha la Kuliombea Taifa na Kuhamasisha  amani linalofanyika katika Ukumbi wa Masai Laugwa uliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani  Pwani.

Alisema mifarakano au choko choko zinapotokea kwa upande wowote ule Viongozi wa Kidini lazima wawe tayari kupatanisha na sio kutumia dhamana yao kuwa wararuaji huku wakielewa kwamba kazi wanayofanya ni wito kutoka kwa Muumba wao.

Balozi Seif alieleza kwamba amani na utulivu wanaojivunia Watanzania walio wengi kwa miaka mingi sasa ni miongoni mwa neema zinazopaswa kutumiwa vizuri na wananchi wa rika zote.

Mapema Askofu Sedrick Ndonde wa Kanisa la Restoration { Restoration Bible Church } alisema Taifa hivi sasa limekuwa na cheche hatarishi inayoonekana kuchochea  choko choko za Kidini, kisiasa pamoja na vitendo vya kigaidi.

Alisema hali hiyo yenye kwenda sambamba na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya inasababisha mfumko wa uhalifu unaowafanya wananchi waendelee kuishi katika maisha ya mashaka na hofu.

Alifahamisha kwamba baadhi ya watu wamekosa uzalendo  kwa kutaka kunufaisha matundo yao. Hivyo ni vyema kwa  Jamii isikubali amani iliyopo nchini  ikachezewa na kuyayuka kama barafu.

Tamasha hilo lilipamba kwa njimbo mbali mbali zilizotayarishwa na kwaya za madhehebu mbali mbali wakiongozwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za injili akiwemo Noel Pascol,Stela Joel pamoja na Dr.Magret Sdoris Kongera.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiingia ndani ya Ukumbi wa Masai Laugwa Wilaya ya Bagamoyo kuzindua Tamasha la Kuliombea Taifa Amani lililoandaliwa na Kanisa la Restoration { Restoration Bible Church } .Kulia ya Balozi Seif ni Makamu Askofu Mkuu wa Restoration Bible Church Tanzania Askofu Sedrick Ndonde na kushoto yake ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Nd. Ahmed Kipozi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilizindua rasmi Tamasha la kuliombea Taifa Amani hapo katika Ukumbi wa Masai Laugwa Wilayani Bagamoyo. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Nd. Ahmed Kipozi na Kushoto yake ni Makamu Askofu Mkuu wa Restoration Bible Churh Tanzania Askofu Sedrick Ndonde. 
Muimbaji wa Nyimbo za Injili Kutoka Mkoani Morogoro Dr. Magereth Isdori Kongera kati kati akiwa na wana kwaya wenzake kwenye Tamasha la Kuliombea Taifa Amani hapo Ukumbi wa Masai Laugwa Wilayani Bagamoyo.
Baadhi ya waumini wa madhehebu mbali mbali ya Dini ya Kikristo waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha la Kuliombea Taifa Amani lililofanyika Masai Laugwa Bagamoyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...