Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akikanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari Gazeti hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakifutailia kwa makini taarifa toka Balozi Seif Ali Idd. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma. 

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd amekanusha madai mbalimbali yaliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014 ambalo liliandika kuwa ‘Siri zavuja za AG Zanzibar kujiuzulu’.

Akikanush taarifa hizo, Mhe. Balozi Idd amesema kuwa Mhe. Othman alitakiwa ashiriki katika kamati kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Zanzibar lakini kutokuwepo kwake katika Kamati sio kikwazo cha kupatikana kwa Katiba, kwani waliokuwepo ndani ya kamati kwa upande wa Zanzibar walitosheleza kuiwakilisha Zanzibar kikamilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. NAFIKIRI ZANZIBAR OMBENI KULA YA MAONI YA NDIYO AU HAPANA KAMA SCOTLAND HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WA UBISHI

    ReplyDelete
  2. TUMESHAOMBA SANA KAKA HAPO JUU ,SEMA TU WATANGANYIKA HAMUTAKI HILO KWA KUWA MNAJUWA FIKA WAZANZIBAR WANATAKA MCHI YAO ,,,WALE VIONGOZI WA UAMSHO WAPO NDANI KWA SABABU MOJA WAPO NI HIYO KUTAKA ZANZIBAE YENYE MAMLAKA KAMILI ,SIO JENGINE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...