Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nnne kulia) akiwepo na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume wakijumuika na waisalmu katika kumswalia Marehemu aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan katika Msikiti wa Mchekeni Magomeni Mjini Zanzibar leo na Kuzikwa kijijini kwao Makunduchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ALhaj Dk. Mohamed Gharib Bilali waliungana na wananchi mbali mbali katika maziko ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan aliyezikwa kijijini kwao Kipunguni Makunduchi jana.
Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofika nyumbani kwa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwapa pole wafiwa leo kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Ndugu wa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipofika kuwapa pole wafiwa nyumbani kwa marehemu Magomeni Mjini Zanzibar leo kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
Baadhi ya akina mama walioshiriki katika mazishi ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Iddi Pandu Hassannyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja jana.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inna lilahi wa inna ilayhi rajiun, pole sana wafiwa hii ni safari isiyoshaka kwetu Sote. muhim tujiandae kwa ajili ya huko tuendako tusijisahau kwa vyeo na Mali. mwenyezi mungu amsamrh makosa yake na amlaze mahali pema peponi. Amiin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...